MAELFU ya waombolezaji jana walijitokeza kumzika aliyekuwa Mhariri Mkuu wa
gazeti la Jambo Leo linalochapishwa na Kampuni ya Jambo Concepts Limited, Willy
Edward (38), aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita mjini Morogoro.
Ibada ya mazishi ya Willy iliongozwa na Askofu wa Kanisa la Kianglikana, Dayosisi ya Mara, Helikia Omindo, aliyesaidiwa na Askofu wa Dayosisi ya Rorya, John Adiema.
Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi, Askofu Adiema, aliwataka waombolezaji kujiweka sawa katika maisha ya kiroho ili mauti yatakapowafika wakati na siku wasiyoijua wawe wamejiandaa katika ufufuo wa wenye haki.
Akizungumzia wasifu wa marehemu, baba mzazi wa Willy, Edward Ogunde, alimwelezea mwanae kuwa ni mtu aliyefanya mambo yake kwa umakini huku akitawaliwa na hulka ya upole.
Mzee Ogunde ambaye ni mwalimu mstaafu, alisema msiba wa Willy ni somo kubwa kwao wao kama wazazi na watu wengine kwani katika mazingira ya kawaida mwanaye huyo ndiye aliyepaswa kumzika yeye kutokana na udogo wa umri wake.
Akisoma ujumbe wa Jukwaa la Wahiriri, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda, alimwelezea Willy kuwa mmoja wa wahariri vijana waliofanya kazi kwa umakini na aliyekuwa karibu sana na wahariri wengine.
Akimwelezea marehemu, Kibanda alisema wingi wa watu waliojitokeza wakati wa kumuaga Willy, Kijiji cha Mugumu jana na kabla ya hapo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, ni wazi Willy alikuwa mtu mwema.
“Waswahili wanasema wema wa mtu humfuata hata katika mauti yake. Wingi wa watu waliojitokeza leo hii hapa Mugumu, hata kule Dar es Salaam ni ushahidi kwamba Willy alikuwa mtu wa watu,” alisema Kibanda.
Katika mazishi hayo jana viongozi mbalimbali wa kiserikali na kisiasa walijitokeza kumuaga katika safari yake ya mwisho.
Miongoni mwa viongozi hao ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kapteni mstaafu, James Yamungu, aliyeongozana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana, na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.
Akimzungumzia marehemu, Mgeja alimwelezea Willy kama mhariri mcheshi, na mtu aliyekuwa tayari kusikiliza na kukubali kushauriwa.
Katika msiba huo Jukwaa la Wahariri mbali na Kibanda liliwakilishwa na Mhariri Mkuu wa gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam, Jane Mihanji, na Mhariri wa gazeti la Mtanzania Jumapili, Revocatus Makaranga.

No comments:
Post a Comment