KageraWANANCHI wa Kijiji cha Nyakabango, Tarafa ya Kimwani, wilaya Muleba, mkoani
Kagera wamechoma nyumba ya mtendaji na mwenyekiti wa kijiji hicho na kuharibu
mali zenye thamani ya zaidi ya sh milioni baada ya viongozi hao kudaiwa
‘kuchakachua’ mahindi ya misaada yaliyotolewa kwa wananchi hao.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo lililotokea Juni 20 mwaka huu kati ya saa 2:00 hadi saa 6:00
usiku.
Alisema kabla ya mali hizo kuharibiwa kulikuwa na vurugu za wananchi dhidi ya
viongozi wa Kijiji cha Nyakabango ambao ni Ofisa mtendaji wa Kata Nyakabango
Ansbert Sabinian(52) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakabango Ladislaus Manana
(41).
Alieleza chanzo cha ugomvi huo ni msaada wa mahindi tani 61.5 uliopelekwa kwa
viongozi hao wa kijiji Mei 28 mwaka huu uliotoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Muleba lengo likiwa ni kugawa kwa wananchi na zoezi hilo lilifanyika.
Alieleza kwamba Juni 19 viongozi waligawa mahindi hayo katika Kitongoji vya
Rwenkara na kesho yake waligawa vitongoji vya Nyamagojo na Nyakabango kisha
kuwatangazia wananchi kuwa mahindi yamekwisha.
Alieleza kwamba ilipofika majira ya saa 1:00 usiku kulikuwa na minong'ono
kuwa mahindi yamechakachulia na viongozi na kuwa ugawaji wa mahindi hayo
haukufuata taratibu ndipo walipofanya msako na kukuta mahindi lukuki yakiwa kwa
viongozi hao.
Miongoni mwa sehemu walizokuta mahindi hayo ni nyumbani kwa Sabinian (Ofisa
Mtendaji wa Kata) ambako walikuta gunia moja na nusu na kwa Tilusubia (magunia
mawili), ambapo waliyatoa nje na kuchoma nyumba moto.
Walikuta pia magunia 12 ya mahindi nyumbani kwa Mwenyekiti wa Kijiji,
Ladslaus Manana.
Kwa mujibu wa Kamanda Kalangi, uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea na
wanawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni mtendaji na mwenyekiti. |
|
|
No comments:
Post a Comment