Na Mwandishi Wetu
ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano
la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi
wa Royal Village.
Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika
katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.
Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana
watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali
zitakazofanyikia Dar es salaam.
Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona
vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana
wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.
“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi
wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba
wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema
Ritha
Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na
Master Jay. EBSS mwaka huu imedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya
Zantel.
No comments:
Post a Comment