Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Thursday, June 28, 2012
'Hili ni aibu kwa taifa'
SUALA la miili ya wahabeshi 43 kukutwa ukiwa umetupwa katika msitu katika Makao makuu ya nchi yetu huku wengine 82 wakiwa hai ni ya dharau na inaonesha ni jinsi gani upo uzembe na mianya ya rushwa kupita kiasi katika nchi yetu.
Nathubutu kusema hivyo kwa sababu haiwezekani idadi kubwa ya watu hao wote wasafirishwe na kuvuka vihunzi vyote vilivyoko barabarani hadi kufika katika makao makuu ya nchi, ambako wanajua kuwa kuna kikao cha Bunge kinaendelea ni tusi, fedheha kubwa kwa vyombo vyetu vya usalama.
Siamini kweli kama aliyewabeba watu wote hao kwenye kontena kama bidhaa,yalikuwa ni mawazo ya mtu mmoja kama si kwamba ili kuwa njama iliosukwa kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa.Hii ni njama ya kimataifa!
Nadhubutu kusema hivi, kwa sababu, nikiangalia vizuizi vilivyojaa barabara mfano kama mikoa ambayo iko mipakani, hawa watu waliwezaje kupita maeneo hayo bila hata wale askari wa barabarani kupekua hilo lori? Au hata kulitilia shaka?
Mbona magari yanayobeba kahawa, nyara za serikali, abiria hupekuliwa hadi kwenye pindo? Iweje kontena tena iliobeba binadamu isipekuliwe?hapa ndiyo maana nasema kuwa ni siri kubwa tena dharau iliobeba rushwa na tusi kwa taifa letu.
Huu ni unyama na biashara ya binadamu.Serikali inatakiwa kufumbua macho yake, itoke kwenye usingizi wa mbono, kwani kwa hili tulioiona na kulisikia huenda hata bunge letu likalipuliwa na tukawapoteza viongozi wetu.Chonde chonde serikali amuka, chukua hatua.
Kalamu kutoka rorya kwetu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment