Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya DISEJI ambayo
ni kampuni tanzu ya TRETEM, inayomiliki vyuo vya Uandishi wa Habari Morogoro
(MSJ) na Dar es salaam (DSJ), Mzee Andrew Allen Sinamtwa amefariki dunia Juni
18, 2012.
Taarifa iliyotolea na Mtoto wa Marehemu, Richard
Sinamtwa, ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusino wa Kampuni ya Tumbaku
Morogoro, (TLTC), mazishi ya marehemu yatafanyika Jumatano 20/6/2012, kijijini
kwake Mangalali, wilaya ya Iringa Vijijini,Mkoani Iringa. Msiba wa Marehemu upo
nyumbani kwake eneo la Nane Nane, mjini Morogoro.
Marehemu alizaliwa tarehe 2 Februari, 1938 huko
Kalenga, Iringa. Kati ya mwaka 1950 na 1953 alipata elimu ya sekondari
Malangali, Iringa. Mwaka 1954 hadi mwaka 1956 alipata mafunzo ya ualimu katika
Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.
Mwaka 1957 alifundisha shule ya kati (District School)
Tinde huko Shinyanga. Kisha alijiunga na shirika la Reli la Afrika Mashariki
mwaka 1958 ambapo alifanya kazi nalo hadi Mwaka 1993 alipostaafu kazi na kuanza
kujishughulisha na vyuo vya uandishi wa habari katika mtandao wa
TRETEM.
Marehemu amekuwa alisumbuliwa na Saratani ya Ini tangu
mwaka jana, ambapo aliwahi kupelekwa nchini India kwa matibabu na aliporejea
alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam hadi umauti
ulipompata.
Marehemu ameacha mke, watoto 9 na wajukuu kadhaa.
No comments:
Post a Comment