BAADA ya nishati ya mafuta ya taa kuadimika katika Manispaa ya Bukoba kwa takribani mwezi mmoja na wiki mbili hatimaye nishati hiyo imeanza kupatikana leo mjini hapa kwa kusua sua.
Katika uchunguzi uliofanywa na blog hii leo asubuhi takribani vituo viliwi vilikuwa na nishati hiyo kati ya vituo vinane vinavyouza mafuta ya taa mjini hapa.
Mmoja ya kituo ambacho blog hii kimeshuhudia wananchi wakienda kununua nishati hiyo ni Kanoni Filling Station kilichoko katika barabara kuu iendayo nchi jirani ya Uganda.
Kwa kipindi kirefu wakazi wa Manispaa ya Bukoba na vitongoji vyake walikosa nishati hiyo, ambapo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa na nishati hiyo walipandisha bei yake kutoka sh. 2280 kadi 3500 kwa lita moja tofauti na bei elekezi iliotolewa na serikali.
No comments:
Post a Comment