MREMBO Noela Michael (19), usiku wa kuamkia jana
alifanikiwa kutwaa taji la Tabata 'Miss Tabata 2012 katika shindano
lililofanyika kwenye ukumbi wa Da’ West Park jijini Dar es
Salaam.
Noela ambaye awali alibwagwa katika kuwania taji
la talent aliweza kuwafunika warembo wengine 18 waliokuwa wanawania taji hilo
lililokuwa linashikiwa na Faiza Ally.
Noela alizawadiwa shilingi 500,000 na king’amuzi
iliyolipiwa miezi sita iliyotolewa na Multichoice.
Nafasi ya pili katika shindano hilo ilikwenda kwa
Diana Simon (20) aliyeshinda Sh 500,000 watatu ni Wilhemina Mvungi (21)
alizawadiwa Sh 350,000), wanne ni Phillos Lemi (19) na Suzzane Deodatus (20)
alishika nafasi ya tano.Wote wawili walizawadiwa Sh 200,000 kila
moja.
Warembo hao watano wataiwakilisha Tabata katika
mashindano ya Kanda ya Ilala yatakayofanyika baadaye mwaka
huu.
Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya 10
walikuwa ni Angel Kisanga (22), Khadija Nurdin (18), Haika Joseph (18), Queen
Issa (20) na Neema Saleh (18). Wote walizawadiwa Sh 100,000 kila
moja.
Queen Issa alifanikiwa kutwaa taji la mrembo
mwenye kipaji cha kucheza huku Mercy Mlay akiteuliwa kuwa mrembo aliyekuwa na
nidhamu ya juu tangu kuanza kwa shindano hilo. Queen na Mercy kila moja
alizawadiwa Sh 100,000.
Warembo awliyosalia walipata kifuta jasho cha Sh
50,000 kila moja.
Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa
bendi ya Mashujaa, Mashauzi Classic iliyoko chini ya Isha Ramadhani Mfalme na
Costa Sibuka.
Shindano hilo iliandaliwa na Keen Arts na Bob
Entertainment na kudhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated
Communications, Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters,
Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady
Pepeta.
No comments:
Post a Comment