Tuesday, June 5, 2012

Mtikisiko wa uchumi wakwamisha miradi mikubwa ya barabara Kagera-MASSAWE

                        

 Meneja wa mkoa wa wakala wa barabara (TANROADS)mkoa wa Kagera,  Bw.Johnny Kalupale akitoa ufafanuzi juu ya masuala ya utekelezaji wa miradi ya barabara mkoani Kagera, kulia ni mkuu wa mkoa wa Kagera Fabian Massawe,anaye ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila na wa mwisho  Bw.Hussein Sei.


Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera waliohudhuria katika kikao hicho.

Baadhi ya waandishi wa habari  nao hawakuwa nyuma katika kupata habari kwa ajili ya kuwahabarisha wananchi.

                                                      Na Theonestina Juma, Bukoba
 BAADHI ya watendaji katika halmashauri Mkoani Kagera wameelezwa kuwa ndiyo chanzo cha barabara za mkoani hapa kujengwa chini ya kiwango.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa Kagera ,Kanali Fabian Massawe wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mjini hapa.
 Alisema imefikia hatua sasa watendaji hao wasio waaminifu kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kuwezesha barabara hizo kujengwa kwa kuzingatia viwango vinavyostahili kulingana na utaratibu wa ujenzi wa barabara.
 Kanali Massawe alisema Watendaji hao wanatakiwa kulinda na kuheshimu dhamana waliopewa na serikali ya kuhudumia wananchi.
 Aidha aliwataka viongozi kuhakikisha wanakuwa wakali kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kudhibiti pindi tatizo hilo la usimamizi mbovu unapojitokeza lengo kulinda
barabara zao.
 "Muwe na macho ya kutazamaza kama mwewe na wa kuchukua hatua na sio kusubiri kutoa taarifa kwenye vikao vya bodi ya barabara wakati hakuna hatua zilizochukuliwa" alisema.
 Katika hatua nyingine, Kanali Massawe alisema ukosefu wa fedha kutokana na mtikisiko wa uchumi umefanya baadhi ya miradi mikubwa wa ujenzi wa barabara za mikoa na kuu zinazojengwa mkoani hapa kusuasua.
 Alisema barabara ya Ushirombo hadi Rusahunga kilomita 110 inayojengwa kwa thamani ya sh.bilioni 114.6 kwa ufadhili wa umoja wa Ulaya (EU) unatarajia kukamilika mwakani na kwa utekelezaji wake umefikia asilimia 42.7 ambapo nayo kwa sasa imesimama kutokana na ukata wa fedha.
  Alisema hiyo muda wa utekelezaji wake ni miezi 39 kutoka   Mkoa wa Geita hadi
Shinyanga imesha kamilika kilomita 36 kati ya 58 na kwa Kagera imekamilika kilomita 11 kati ya 52 ya mradi huo  ambao nao umekwama kutokana na ukosefu wa fedha tangu mwa 2010.
 Hali hiyo pia imekumbabarabara ya Kyaka Bugene kilomita 51 inayojengwa kwa fedha za ndani kulingana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010.Alisema hadi sasa
utekelezaji wa barabara hiyo imeshafikia asilimia 26 tu ambapo muda wake umeshapita kwa asilimia 57.

No comments:

Post a Comment