Thursday, March 21, 2013

LHRC yatoa mafunzo kwa waangalizi wa haki za binadamu wapatao 252 DSM


Baadhi ya waangalizi wa haki za binadamu na wasaidizi wa kisheria wakiwa katika mafunzo ya siku tatu yanayohusu mchakato wa uundwaji wa mabaraza ya katiba mpya nchini,mafunzo ambayo yanaratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadmu.

Mratibu wa dawati la katiba kutoka Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC Bi.Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo.

Sunday, March 3, 2013

Mgogoro wa Meya wa Bukoba, Dkt Amani na Mbunge Kaghasheki washinda CCM sasa waomba serikali kuu kupitia Waziri Mkuu Pinda kuunda tume


Na Theonestin Juma
CHAMA cha mapinduzi taifa kimesema mgogoro wa kisiasa katika  Manispaa ya Bukoba umevuka mpaka wa Chama na hivyo kimemwangiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia wizara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuunda tume  kutoka wizarani  ili kuja Bukoba kuchunguza tuhuma zinazoelekezwa kwa Meya wa Manispaa hiyo, Dkt. Anatory Amani.
Kauli  hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) itikati na uenezi taifa, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari  uwanja wa ndege mjini hapa akiwa safarini kuelekea Jijini Dar Es Salaam baada ya kufanya ziara yake  siku moja mjini hapa baada kusikia mgogoro unaondelea ndani ya manispaa hiyo ya baadhi ya madiwani kususia vikao na hivyo kuathiri utendaji ndani ya manispaa hiyo.
 Nnauye alisema mgogoro ulipo katika manispaa ya Bukoba umevuka mpaka na hivyo inahitajika serikali kuu kuingilia kati.
Alisema mgogoro huo umeathiri vikao vingi vya CCM, jambo ambalo amesema kuwa limesikitisha chama hicho taifa na hivyo kuhitajika nguvu za ziada kuondoa mgogoro huo.
Alisema katika mazungumzo yao na baadhi ya madiwani hao wametakiwa kurudi na kufanya vikao kama kawaida  kwa maendeleo ya jamii kulingana na utaratibu na kanuni za Manispaa hiyo.
Alisema CCM taifa kinasikitishwa na kufedheheshwa na mgogoro unaoendelea katika manispaa ya Bukoba, kwani hauna tija kwa yeyote, wala kwa chama, kwa wananchi hata kwa watu wanaoshikiriki katika mgogoro huo.
Alisema kuna tuhuma nyingi ya Meya kuhusiana na soko, kituo cha mabasi, viwanja na uendeshaji wa halmashauri na hivyo tume ikija inayo mamlaka ya kuchunguza na kutoa taarifa.
Alisema taarifa ya tume hiyo ikiamilika itawekwa hadharani kwa sababu maneno hayo yametoka ndani na kwa sasa yako nje kwa hiyo ni vizuri wananchi wakajua.
Alisema wakati wa kuchunguza wanayo mamalka kama tume pamoja na mambo mengine wanaweza kulazimika kusimamisha baadhi ya watu kwa ajili ya kupisha uchuguzi huo lakini wao wataangalia sheria zinasemaje.
Kuhusiana na vipeperushi vinavyoendelea kutolewa mjini hapa alisema kuwa vipeperushi hivyo vimekuwa vikigawa wananchi na viko katika mrengo wa kugawa watu kidini.
Alisema kutokana na vipeperushi hivyo, chama hicho kimeagiza serikali kuwatafuta watu wanaotengezeza vipeperushi hivyo ili kuweza kuchukuliwa hatua na kuwa anamaamii kuwa hakuna atakayepona katika hilo hata kama ni wanachama wa CCM
“Hatuwezi kuvumilia masuala kama haya, kama ni wanachama wetu lazima tutawachukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na chama cha CCM”alisema
Kuhusu baadhi ya madiwani kuwekwa mfukoni na baadhi ya watu, alisema mgogororo huo umevuka mpaka wa chama ndiyo sababu wamweo mba tume inge ichunguze suala hilo.
“Mgogoro huu ulikofikia kwa sasa umevuka mpaka wa chama ndiyo sababu sasa tunataka tume ije ichungue mambo kama hayo ya baadhi ya mafiwani kuwekwa ndani ya mfuki wa mtu, wao ndiyo watatuambia ukweli, ama hawa madiwani wanaamua kufanya hivhyo kwa utashi wao’alisema Nnauye.
Tume utagundua kama kuna fedha zimechakachuliwa, au msingi wa mgogoro huu ni nini, hiyo timu inatao majibu yake.
Kuhusu athari ambayo mgogoro huo umeleta ndani ya chama Bw. Nnauye alisema kuwa ni pamoja na chama sio kitu kimoja , watu wamegawanyika, nah ii ni kutojna na madiwani wa CCM ndiyo wengi,
Halikadhalika alisema mgogoro huo umeathiri utekelezaji wa ilani ya ccm ya uchaguzi mwaka 2010 kwa sababu bajeti isipotishwa pesa hazitatoka kwa wakati na hivyo miradi mingi itakwama, kuanza kutekelezwa, pia waathirika wakubwa ni wananchi, mfano kama huduma ya maji , madawa, shule zitakosekana.
‘Kutokana na hali hii, ndiyo maana kwa sasa inahitajika nguvu kubwa, … zaidi itumike ili kumaliza mgogoro huu, kwani utaathiri utekelezaji wa ilani ya uchanguzi wa CCM “alisema
Alisema mgogoro huo ndiyo chanzo cha kuzaa vipeperushi vilivyozaa mitaani ya  unalenga kugawa wananchi wa manispaa ya Bukoba. Na ndiyo maana vikao vikitaka kufanyika watu hudhuria ili kuja kuangalia kwa sababu watu wamegawanyika.
“Tumeigawa jamii yetu kutokana na mgogoro huu, unakuta kundi moja linapita upende mwingine na lingine upande moja wanaanza kuzomeana, tukiendelea hivyo wanaishi  kama watu ambao si wa eneo moja, si watu ambao walikuwa wanakubalina, litafanya Bukoba lisiwe eneo nzuri la kuja kupumzika”alisema
Alisema wakati mgogoro huo unaanza si kweli kuwa Chama kilikaa kimya bali kuna hatua zilizochukuliwa na kwamba si kwamba kila mgogoro unapoanza lazima CCM taifa liingilie kati, bali pale ambapo ngazi ya chini inaposhindwa ndipo taifa huingilia kati.
“Sisi hatuna utamaduni wa kuhamisha babu na vijukuu katika sehemu moja ya migogoro kama ilivyo kwa wapinzani wetu, sisi tunautaratibu wetu,… sisi sio chama cha harakati … sisi tunautaratibu wa kushughulikia migogoro”alisema
Mgogoro ndani ya chama ikizimgatiwa kuwa mwaka 2014 wanaingia katika uchanguzi wa serikali za mitaa, alisema kuwa sehemu ambapo kuna mgogoro ni afya .
Alisema malumbano na mvutano huo unatewgemea pia kutofautiana kule unahitimishwaje , hivyo kuamua watashindishaje ni kuangalia ni ni namna walvyotafautiana.
Alisema “wenzetu wale ambao ni wapinzani wetu wasubiri tu ushindi wa kibunga 2015, kwani watu wamewachoka na wamewaona walivyo wakiwa bungeni.
Aidha aliwapa ushauri wapinzani kuwa miaka mingi  Tanzania wamekuwa na vyama vya upinznai vya kukosa na sio kuelekeza na kuleta sera mbadala.
Katika mfumo wa vyama vingi ukiwa na vyama vya nam,na hiyo, vitabaki kuwa  vya upinzani kwa muda mrefu kwa sababu wao wakikosoa wao wanakwenda kurekebisha na wananchi wanazidi wakuwapenda.
Ukitaka kushika dola toa kitu mbadala wenzao wanafanya A’ wewe sema ukipewa madaraka utafanya B’ haitoshi kukosoa A peke yake bila kutoa mbadala sasa wenzetu kwa utaratibu huu tunawaombea maisha mema ya kuendelea kuwa wapizani, wafanye kazi nzuri ya kutukosoa ,ya kupiga kelele, kupata ruzuku kwa sababu ndiyo wanayoitaka na sisis tumepewa kazi ya kupanga mikakati ya maendeleo”alisema
Mwisho.