Saturday, June 23, 2012

Kimya kingi....Jennifer Mgendi kutoa filam mpya' Chai Moto'

 





  

Mwimbaji Mkongwe wa Nyimbo za Injili Tanzania Jennifer Mgendi anatarajia kutoa Filamu nyingine aliyoipa Jina la “Chai Moto”.
Akizungumza na Blog hii kuhusu Filamu hiyo,Jennifer anasema ameamua kutoa Filamu hiyo baada ya kuona Misukosuko ya Kimaisha imezidi kuongezeka Miongoni mwa Watanzania. Lengo la kutoa Filamu hii, ni kuonyesha namna gani Watanzania wengi wanakumbwa na Misukosuko ya Kimaisha kila inapoitwa leo.

Kwahiyo nategemea Filamu hii itakuwa kama njia ya kuwanasua watu katika Misukosuko hiyo ambayo si Mpango wa Mungu wetu sisi tuishi hivyo.” – Alisema Jennifer Mgendi Filamu hiyo iliyowashirikisha Mastaa kibao wa Bongo Movies kama Mussa Banzi, Yvone Cherryl a.k.a Monalisa, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Christina Matai, Jennifer Mgendi mwenyewe, na Wengine kabao inatarajiwa kutoka Mwezi ujao kwani kwa sasa ipo katika hatua ya Mwisho ya Kuhaririwa. Filamu hii imeongozwa na Mgeni Khamisi, Mussa Banzi, na Chrissant Mhengga. Kuhusu Masuala ya Uimbaji Jenipher amesema, kwasasa yupo kwenye Mpango wa Kutengeneza Video ya Albam yake ya “Dhahabu” yenye Nyimbo kama Ukarimu wake, Ulinipa Sauti, Nitafika Lini, n.k itakayotoka Mwezi wa Nane Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment