Saturday, June 30, 2012

Jamii ya wafugaji, wawindaji waeleza yale wanayoyataka yawemo kwenye katiba mpya

Familia ya Wafugaji wa Kimasai
ARUSHA

HATIMAYE jamii mbalimbali zikiwemo jamii za wafugaji  pamoja na
wawindaji  wa asili wamefanikiwa kueleza na kujadili mambo mbalimbali
ambayo wanayataka yaweze kuwepo kwenye Katiba mpya.
Ambapo masuala hayo pamoja na michango yao imejikita zaidi  katika
masuala ambayo ni muhimu kwao kama vile ardhi,fidia, pamoja na
mchakato mzima wa ulinzi  ndani ya jamii zao.
Wadau hao waliysema jana katika uzinduzi wa chombo kilichoundwa ili
kutekeleza maazimio ya mkutano  mkubwa wa viongozi mbalimbali wa jamii
za kifugaji uliofanyika chini ya asasi ya Pingos na Alapa mwishoni mwa
 mwaka jana
Pia walisema kuwa ndani ya katiba mpya kuna takiwa kuwe na suala zima
la usimamizi wa masuala ya ,msingi hasa kwa wafugaji kama
vileusimamizi wa ardhi mikononi mwa taasisi za kuwakilisha kwa kuwa
sasa kuna tofauti kubwa sana hasa kwenye katiba hiyo mpya kwa kuwa
suala zimala usimamizi upo chini ya vyombo vikubwa sana vya Serikali.

Akiongea na wadau hao mratibu wa katiba initiative, (KAI),  bw William
Olenasha alisema kuwa kwa sas ni vema kama jamii hiyo ya wafugaji
ikahakikishea kuwa inawakilisha vema matatizo ambayo yana wakabili wao
hasa wawindaji wa asili ambapo pia wanatakiwa kuhamasiasha watu
kuhakikisha kuwa wanatoa maoni yao hasa kwenye mchakato wa katiba
mpya.

No comments:

Post a Comment