Monday, June 18, 2012

Kocha wa Twiga Stars Mkwasa aachana na Twiga

Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Baada ya timu ya Twiga Stars kuondolewa katika michuano ya kwenda katika fainali za Afrika kwa Wanawake zitakazopigwa mwaka huu huko Guinea ya Ikweta, kocha wake, Bw. Charles Mkwasa ameandika barua ya kujiuzulu kuifundisha tena.
Kwa mujibu wa Bw. Mkwasa imefika wakati sasa ya kuwapisha makocha wengine wazalendo kuifundisha timu hiyo ya wanawake.
Hatua hiyo imekuja siku mbili tu baada ya Twiga Stars kuondolewa katika michuano hiyo na timu ya Ethiopia ambao katika mchezo wa awali uliwafunga timu hiyo 2-1 nchini Ethiopia na juzi Jumamosi ilifungwa kwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani.

No comments:

Post a Comment