Sunday, June 10, 2012

Waziri Saitoti na Naibu wake wafa katika ajali ya Helkopta Kenya

Prof George Saitoti
Prof George Saitoti
 Waziri wa Usalama wa Ndani ,Profesa George Saitoti, na Naibu wake, Bw.Orwa Ojode, wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Kibiku karibu na mji wa Ngong, takriban kilometa ishirini kutoka mji wa Ngong.
Abiria wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo wanaarifiwa kuteketezwa kwa kiasi wasichoweza kutambulika.
Kamishna wa polisi Mathew Iteere anaarifiwa kulekea katika eneo la ajali hiyo.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema ndege ilishika moto ilipogusa ardhi kwenye eneo la msitu wa Ngong.
Bw. Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao.

No comments:

Post a Comment