Balozi wa Ukraine Volodymyr Butiaha akiwasilisha
hati za Utambulisho
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete leo amepokea hati za mabalozi watano wanaoziwakilisha nchi zao hapa
pamoja na kupokea wajumbe wawili maalum waliotumwa na marais Salva Kiir wa Sudan
Kusini na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mabalozi
waliowasilisha hati za utambulisho ikulu ni pamoja na Mhe.Domingo Lucenario wa
Phillippines, Mhe.Volodymyr Butiaha wa Ukraine,Mhe.Beyene Russom Habtai wa
Eritrea, Mhe.Kingsley Saka Karimu wa Ghana pamoja na Mhe.Gil Haskel wa
Israel.
Wajumbe walioleta salamu
maalum kutoka kwa marais wao ni pamoja namhe.Raymond Tschibanda ambaye ni Waziri
wa Mambo ya nchi za nje wa DRC na Mhe.Nhial Deng Nhial ambaye ni waziri wa mambo
ya nchi za nje wa Sudan ya Kusini. (picha zote na Freddy Maro)
|
No comments:
Post a Comment