Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya
Kiarabu ya Saharawi Mhe.Mohamed Abdelaziz picha ya
waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Hayati Mwalimu Julius Nyerere
na Hayati Abeid Karume wakibadilishana hati za
muungano muda mfupi baada ya Rais Kikwete na mgeni wake kumaliza mazungumzo
rasmi ikulu jijini Dar es Salaam leo.Mhe.Mohamed Abdelaziz
Rais wa Jamhuri ya kiarabu ya Saharawi aliwasili nchini jana jioni
kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa
Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi Mhe.Mohamed Abdelaziz leo asubuhi.(picha na
Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment