WIZARA ya Nishati na Madini imesema kwa sasa imejipanga
kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini, hususan katika kuboresha shughuli
zao.
Akizungumza na Fullshangweblog jijini Dar es Salaam
jana, Naibu Waziri wa sekta hiyo Steven Masele alisema kwamba mkakati huo
umekuja siku chache baada ya kubaini kuwa wachimabji hao wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa vitendea kazi.
Alisema kwamba moja ya ongezeko la uchumi wa nchi
unatokana na madini, hivyo kuna haja ya kuliangalia kundi hilo kwa lengo la
kupanua pato sanjari na ajira kwa wazawa.
Aidha, alichanganua kuwa wigo wa wizara hiyo umekuwa
kwa asilimia 3.3 tofauti na awali ambapo ulikuwa asilimia 0.6.
"Wachimbaji wadogo wamekuwa wakiendesha shughuli zao
katika wakati mgumu sana, hasa kwa kukosa vitendea kazi vya kuaminika jambo
ambalo limekuwa likisababisha wengi wao kufariki wakiwa migodini"alisema
Masere.
Naibu huyo, alivitaja baadhi ya vifaa ambavyo
wachimbaji hao wanavyohitaji kuwa ni pamoja na mashine za kuingiza na kutolea
hewa chafu, ya kuingia na kutoka wakati wakiwa migodini.
No comments:
Post a Comment