Saturday, June 9, 2012

Radi yateketeza familia yote yauwa mama na wanae watano Kyerwa



Na Theonestina Juma, Bukoba
WATU sita wa familia moja mama na wanae watano wamefariki dunia kwa kupigwa na radi katika kijiji cha Kihinda kata ya Kibingo  katika wilaya mpya ya Kyerwa  Mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini Bukoba kutoka wilayani Kyerwa  na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Phillip Kalangi tukio hilo limetokea Juni 8, mwaka huu saa 10.30 jioni katika kijiji cha Kihinda  kata ya Kibingo tarafa ya Kaisho Murungo wakati watu hao wakiwa ndani ya nyumba yao.
Watu waliouawa kwa kupigwa radi wamejulikana kuwa ni pamoja na  mama wa watoto hao Bi.Kevina Kamachoma mkazi wa kijiji cha Kihinda.
Watoto wake waliouawakwa kupigwa na radi ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Kihinda ambao ni pamoja na Alan Aaron darasa la tano, Kamagambe Jofrey darasa la kwanza na Kazungu Emmanuel darasa la sita.
Wengine pamoja na watoto wawili wanaosadikiwa kuwa wana umri kati ya mwaka mmoja na miwili ambao majina yao hayajapatikana.
Imeelezwa kuwa radi hiyo ilipiga nyumba ya nyasi ambayo iliwaka moto na kuwauwa watu sita waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo,.

Alisema tukio hilo liko nje ya uwezo wao na hivyo kuomba watu wenye utaalamu wa masuala ya radi kujitokeza ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi hao namna ya kuepukana na ajali za radi. 
Hii ni mara ya kwanza radi kuua wananchi tangu mwaka huu uanze mkoani hapa, licha ya katika kuwepo kwa matukio ya radi kupiga maeneo mbali mbali mkoani hapa hasa shule za msingi na sekondari.

No comments:

Post a Comment