Arusha
VYUO vikuu 60 zikiwemo
taasisi za elimu ya juu na wadau wa vifaa mbalimbali vya elimu kutoka
nchi za Afrika mashariki wanatarajia kushiriki katika
maonyesho ya huduma na bidhaa zao yatakayofanyika mwezi ujao mjini
Arusha.
Mratibu wa maonyesho
hayo Peter Oguwi amesema maonyesho hayo yatakayoanza julai 10 hadi 14 yatafanyika katika
viwanja vya nane nane njiro.
Pia
nyatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika mashariki ikiwemo India
maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza kufanyika na
yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500.
Oguwi amesema lengo la
maonyesho hayo ni kutangaza huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo program
mbalimbali ilikuwafanya wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala ya
kukimbilia nchi za nje hivyo maonyesho hayo yana tarajia kufanya
mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ya juu.
Waziri wa elimu na
ufundi Shukuru kawambwa anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 11 mwaka
huu Jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment