Saturday, June 23, 2012

ICTR yakubali kuhamishiwa kesi ya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda


Arusha

Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatano imekubali maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ya kuhamishia kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa, Charles Ryandikayo,kwenda kusikilizwa nchini Rwanda, ikiwa kesi ya sita kuhamishiwa nchini humo.

Mahakama iliyotoa maamuzi hayo ikiongozwa na Jaji, Vagn Joensen imeeleza kwamba, kwa kuzingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, imefikia uamuzi wa kuhamishia kesi hiyo nchiniRwanda.

‘’Mahakma imeamua kesi kupelekwa kwenye mamlaka ya Jamhuri yaRwandaili wenye mamlaka hayo kuiwasilisha kesi hiyo mbele ya Mahakama Kuu yaRwandakwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa haraka,’’ inasomeka sehemu ya uamuzi huo.
Imeelezea matumaini yake kwamba’’Jamhuri yaRwanda, kwa kukubali kupokea kesi kutoka mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, itatimiza wajibu wake kwa uaminifu, uwezo na nia njema ya kuendesha kesi hiyo kwa kufuata viwango vya juu vya haki vya kimataiafa.’
’ 
Ryandikayo ambaye alikuwa Meneja wa mgahawa mmoja wa Mubuga katika wilaya ya Gishyita mkoani Kibuye, Magharibi yaRwandaanashitakiwa kwa mauaji ya kimbari, kula njama za kufanya mauaji hayo, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.ICTR imeshatoa maamuzi katika maombi matanokamahayo.

Maombi hayo yanahusu mtu mwingine ambayo bado anasakwa pia, Ladislas Ntaganzwa, meya wa zamani wa wilaya ya Nyakizu, mkoani Butare, Kusini mwaRwandana Bernard Munyagishari, anayedaiwa kuwa kiongozi wa wanamgambo wa Interahamwe mkoa wa Gisenyi, Kaskazini ya Rwanda.Lakini upande wa utetezi unatarajiwa kupinga maamuzi hayo.

Maombi mengine matatu ya aina hiyo ambayo yameshatolewa uamuzi na ICTR yanawahusu, Mchungaji Jean Uwinkindi na watuhumiwa wawili ambao nao bado wanasakwa ikiwa ni pamoja na Fulgence Kayishema na Charles Sikubwabo.

Maombi mengine mawili ya aina hiyo ambayo yapo mbele ya mahakama yakisubiri uamuzi ni pamoja na ya Aloys Ndimbati, meya wa zamani wa Gisovu na Luteni Kanali Pheneas Munyarugarama, kamanda wa zamani wa kambi ya jeshi ya Gako, wilayani Kanzenze katika mkoa wa Kigali Vijijini.

No comments:

Post a Comment