WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha, juzi walivamia ofisi
binafsi ya Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Stanley Hotay na kufyatua risasi
kabla ya kupora fedha taslimu zaidi ya milioni 10 pamoja na vitu
mbalimbali.
Habari zilizopatika juzi jioni na kuthibitishwa na Askofu Hotay mwenyewe, zilieleza kuwa watu hao waliokuwa na bastola walivamia ofisi hizo za shirika lisilo la kiserikali la HEREF Life jana mchana muda mfupi baada ya kesi ya kumpinga Askofu huyo kuahirishwa.
“Ni kweli nimepata taarifa kuwa majambazi yamevamia ofisini kwangu na kupora fedha na vitu mbalimbali, najaribu kuwasiliana na wafanyakazi wangu ili nipate maelezo zaidi lakini nimeshindwa kutokana na simu zao zote kutopatikana, sijui kama pia zimeporwa,” alisema Askofu Hotay
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma alikosema yuko kikazi, Askofu Hotay alisema hajui lengo la uvamizi huo kama ulikuwa kuiba au kumtafuta yeye binafsi na kuviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kutafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake.
Mmoja wa watu walio karibu na Askofu huyo aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, alisema kabla ya tukio hilo mhasibu wa ofisi hiyo aliyejulikana kwa jina la Neema Mbonea akiwa na dereva ambaye jina lake halikupatikana, walitoka benki.
Chanzo hicho kilisema kwamba, wakiwa ndio wanaingia ofisini, ghafla watu wawili mmoja akiwa na
bastola na mwingine nondo waliwavamia na kuchukua mfuko uliokuwa na fedha kabla ya kumpiga kwa nondo mhasibu huyo katika bega lake la kulia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo chake.

No comments:
Post a Comment