Thursday, June 21, 2012

Baada ya Mkwasa kubwaga manyanga Twiga stars wachezaji hao warushiwa kombora ya kufanya ngono ya jinsia moja wawapo kambini

BAADA ya Timu ya taifa la Wanawake Twiga stars kuondolea katika kushiriki katika fainali ya kwenda Iqeuetorial Guene kumeibuka tetesi kuwa aadhi ya wachezi hao wamekuwa wakifanya ngono ya jinsi moja.
Tuhuma hiyo ambayo ni nzito na ya siri hufanya wawapo kambini ambapo imeelezwa kuwa ndiyo chanzo cha kiwango cha timu hiyo kushuka.
Hata hivyo, kwa upande wa Afisa Habari wa TFF, Bonfas Wambura alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alisema kuwa hawezi kuthibitisha hilo kwani hadi uchunguzi ufanywe ili kubaini kama ni kweli ama la.
Tuhuma hizo zimeibuka siku mbili tu baada ya kocha wa timu hiyo, Charles Mkwasa kubwaga manyanga ya kuongoza timu hiyo, ya wanawake ambayo mara nyingi imekuwa kama kinda la ndege lisilokuwa na wazazi wake kwani mara nyingi timu hiyo ikitaka kwenda kucheza sehemu yoyote lazima viongozi wao wapige mayowe ndipo iweze kuchangiwa  licha ya kuwa timu hiyo pekee ndiyo imewahi kutoa nchi kimasomaso tofauti ya wanaume haina hata mafanikio zaidi ya kubaki kuwa ' kichwa cha mwenda wazimu'.

No comments:

Post a Comment