Mwandishi Wetu Morogoro
WAKULIMA wadogo wa Kijiji cha Kisaki wilayani
Morogoro wameyataja matrekta madogo aina ya ‘Power tiller’ walioyanunua kwa
kilimo kuwa mkombozi kwa wagonjwa hususani wajawazito baada kubadilishwa kuwa
magari ya kuwabeba badala ya kazi ya kilimo.
Hayo yalibainishwa mjini
Morogoro na baadhi ya wakazi kijijini humo wakati wakitoa mrejesho wa
ulaghibishaji masuala yanayorudisha nyuma maendeleo kwa jamii kwenye mkutano
uliowakutanisha viongozi wa Serikali na wananchi wilayani humo.
Mmoja wa
wananchi wa Kijiji cha Kisaki kilichopo wilayani humo, Tatu Maleta alisema kuwa
vijiji hususani kijiji hicho wamekuwa wakikabiliwa na kero nyingi Iikiwamo ya
kukosa usafiri wa uhakika kwa wagonjwa.
Alisema ubovu wa barabara umekuwa
chanzo kikubwa cha kero hiyo na kwamba matukio ya kufariki watu kwa kukosa
huduma za afya ni mengi.“Tunalazimika kutumia matrekta madogo ‘Power
Tiller’kuwapeleka wagonjwa Kituo cha Afya Duthumi kilomita zaidi ya 40’’
alisema.
Akifafanua zaidi alisema kutokana na ugumu wa usafiri wananchi
wamekuwa wakilazimika kutumia ‘Power tiller’ kwa ajili ya kuwawahisha wagonjwa
kwenye kituo hicho.Aidha walisema wangependa kupata elimu inayohusiana na
umuhimu wa katiba ili washiriki vema katika kutunga na iwe na manufaa zaidi
katika maisha yao.
Akitoa ufafanuzi wa mfumo wa mipango ya maendeleo
inavyoandaliwa na jinsi inavyowanufaisha wananchi, Ofisa Maendeleo ya Jamii
kutoka ofisi hiyo wilayani humo, Mary Nyanje mbali na kukiri kuwapo maagizo
kutoka serikalini alisema mipango mingi huanzia ngazi za vitongoji na hatimaye
inapitia vijiji, kata, wilaya, mkoa na hatimaye Taifa.
Mary alisema
mipango inayoanzia taifani ni ile ya kitaifa akitoa mfano wa kilimo kwanza na
mingineo huku ile inayogusa maendeleo ya vijijini na vitongoji akiitaja kuwa ni
pamoja na ile inayohusiana na mipango ya uboreshaji huduma za jamii kama afya,
maji, shule, barabara na masoko.
No comments:
Post a Comment