Na Theonestina Juma, Bukoba
BAADHI ya watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka
(BUWASA) katika Manispaa ya Bukoba wamemlalamikia Meneja wa fedha wa mamlaka
hiyo, Bw.Jacob Laiser kwa kuwanyanyasa pamoja na kuwatolea lugha .
Hayo yamebanishwa jana (leo) na baadhi ya watumishi wa
mamlaka hiyo wakati wakazingumza na gazeti hili mjini hapa.
Wafanya kazi hao walisema kwa kipindi kirefu Meneja fedha
huyo amekuwa ni chanzo cha migogoro katika mamlaka hiyo kutokana na ushauri
wake mbaya kwa Mkurugenzi wa mamlaka hiyo na kwamba hana ushirikiano mzuri
baina ya watumishi wenzake hali inayofanya kukosa ari ya kufanya kazi.
Baadhi ya lugha chafu wanazotolewa na Meneja huyo wa fedha
walidai kuwa ni pamoja na pindi wanapolalamikia mshahara mdogo kutokana na
fedha za kujikimu kuondolewa, huwajibu kuwa kama mtu haridhiki na kiwango hicho
anaweza kumwaajiri kwenye shamba lake la mifugo lilioko katika ranchi ya
Missenyi.
Pia walidai kulingana na utaratibu wa mamlaka hiyo, mtu
husaini mkataba ambapo kila mkataba unapoisha hulipwa kiinua mgongo wake kabla
ya kusaini mwingine ambapo hadi sasa kuna baadhi yao tangu mwaka 2007 hadi sasa mkataba wao wa awali
kwisha na kusainishwa mwingine bado hawajalipwa kiinua mgongo wao wa awali.
“Tulipoanza kudai haki zetu katika vikao vya watumishi wote,
tuliambiwa kuwa tangu mwaka 2007 walifungua akaunti maalum kwa ajili ya kuweka
kiinua mgongo wa wafanyakazi wote ambapo hadi sasa akaunti hiyo haijafunguliwa
na hawajalipwa kiinua mgongo wao”alisema mmoja wao.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili juu ya tuhuma hizo,
Meneja wa fedha huyo, Bw. Laiser alidai kuwa tuhuma hizo ni za siku nyingi na
kwamba hajui ni kwa nini analalamikiwa kwani kama ni haki anawatendea watu
wote.
“Dada yangu, kama kusema nimeshasemwa sana na hao baadhi ya
wafanya kazi hata hili suala tayari walishamwambia Mkurugenzi na kwa sasa
tuhuma hizi zinachunguzwa na wajumbe wa Bodi wa mamalaka hii, lakini tatizo
kubwa sijui”alisema
Malalamiko hayo yameletwa hadi ofisi kwangu, kwa bodi , kwa
Mkurugenzi hadi wizarani nimeshaitwa na kuhojiwa na kujieleza sasa tunasubiria
maamuzi tu kuwa yatakuwa vipi, lakini wanapokuletea malalamiko haya inamaamuzi
ngazi zote hizo walikofikia hawaamini, au mtu akishafikishwa mahakamani lazima
tena ashtakiwe gazetini pia?
Alisema tuhuma za kuwatolewa lugha chafu, hana ushirikiano
nao na anaushauri mbaya kwa mkurugenzi
katika suala la matumizi ya fedha ni maneno ya uongo dhidi yake kwani haelewi hawa watu anawatolea lugha chafu hizo
katika mazingira gani na kwa nini awatukane.
Alisema kama malalamiko juu ya malipo, ni madai yao ya
msingi lakini tatizo linatokana na Mamlaka hiyo kutofikia malengo ya kazi zao,
ofisi haina hela kutokana na kudai madeni mengi nje, lakini kutokana na mawazo
ya watu wengine wao wanadhani kuwa fedha hizo lakini wanatakataa kwa makusudi
kuwalipa.
Alisema hili ni Shirika la umma hawezi kuamua kufanya jambo
lolote bila kushauriana na uongozi lakini haya wanayana ni kero hivyo, hata
kama nikiondoka sidhani kama hao wanaolalamika watachukua hiyo nafasi yangu
bali itatangazwa nafasi hiyo na kuja mtu mwingine.
Naye Mkurugenzi wa BUWASA, Mhandisi Chaggaka Kalimbia
akizungumza na gazeti hili juu ya tuhuma hizo, alidai kuwa mfano lugha chafu
hawezi kuthibitisha wala kushuhudia kwani haieleweki ameyatolea katika
mazingira gani na wapi na huenda wanatoleana mitaani hivyo ni vigumu kwake
kuyaelezea.
Alisema malalamiko hayo yapo, lakini cha muhumu ni watu hao
kuwekwa sawa, kutokana na huenda katika mazungumzo yao wakawa wanataniana
lakini mtu mwenye akaona kuwa ametukanwa.
Kutokuwa na mahusiano na wafanyazi wenzake ni lazima
iangaliwe hao wanavigezo vipi, mfano kama ushauri katika masuala ya fedha, mimi
naweza kumwambia angalie hali ya fedha hata kama nimeidhinisha hicho kiasi alipwe
mtumishi lakini yeye anaweza kuangalia kweli hizo pesa zinapatikana?
Fedha zinapatikana kulingana na hali halisi, hivyo
inapokosekana lazima alipwe hata kwa awamu awamu.
Kuhusu kiinua mgongo wanayoprogramu ya kuwalipa, wameweka
kama madeni lakini yote hayo yanatokana na hali ya upatikaji wa fedha ambapo
kwao yanatokana na mapato tu, ambapo kwa mwaka jana waliwalipa baadhi ya watu
wengine na mwaka huu wanatarajia kuwalipa wengine pesa zikipatikana.
Naye Mwenyekiti wa Bodi BUWASA, Bw. Samuel Rutaguka akizungumza
na gazeti hili alikiri bodi kupokea
malalamiko hayo ambapo kwa sasa wanayafanyia uchunguzi ambapo kwa sasa
wanamwezi mmoja tangu waanze kazi hiyo.
Alisema Kutokana na meneja fedha kuomba likizo ya dharura
kutokana na kuwa na tatizo nyumbani kwao anatarajiwa kurudi kazini Juni 15,
mwaka huu, ambapo ndiye amebaki kuhojiwa
ili kuweza kufunga uchunguzi.
Alisema katika uchunguzi huo, baadhi ya watumishi hawakuwa
tayari kuzungumzia malalamiko hayo kutokana na woga lakini lakini asilimia yao
kubwa walilalamikia mambo hayo hasa kutolewa lugha chafu pamoja na kutokuwa na
ushirikiano nao ambayo yalikuwa ya msingi katika malalamiko yao.
Alisema tangu waingilie kati kutafuta ufumbuzi wa malalamiko
hayo na kuanza kuyachunguza tayari kumeshafanyika vikao vinne, ambapo
wafanyakazi hao wameonekana kuongeza juhudi kufanya kazi tofauti na hapo awali.
Naye katibu wa TUGHE
Mkoa Kagera, Bw. Damas Meja akizungumza na gazeti hili, alikiri kupokea
malalamiko hayo ambapo kwa sasa anasubiri bodi imalize uchunguzi wake na kutoa
majibu ili nao waweze kuangalia ni nini cha kufanya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment