UHABA wa madawati katika shule za msingi na sekondari
umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini,
ikiwemo Shule za Wilaya ya Musoma Vijijini.
Upungufu wa madawati katika
shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia
kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na
mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.
Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha
wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na
wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema.
Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Etaro wakiwa
darasani wakimfuatilia mwalimu. wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini
kutokana na uhaba wa madawati. Add
caption |
No comments:
Post a Comment