Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya klabu, Jangwani. |
KATIBU wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakhim Masu leo
asubuhi amechukua fomu ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya
Yanga ya Dar es Salaam.
Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amewataja wengine waliochukua fomu leo ni Mussa Katabaro, Muzamil Katunzi, Lameck Nyambaya, Edgar Fongo, Ahmad Waziri Gao na Yona Kevela.
Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amewataja wengine waliochukua fomu leo ni Mussa Katabaro, Muzamil Katunzi, Lameck Nyambaya, Edgar Fongo, Ahmad Waziri Gao na Yona Kevela.
Mapema jana, vigogo wengine watatu walichukua fomu za
kugombea nafasi tofauti, hivyo kufanya uchaguzi wa Yanga utakaofanyika Julai
15, mwaka huu uzidi kuwa na msisimko.
Waliochukua jana ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Handeni,
Muhingo Rweyemamu, milionea Abdallah Ahmed Bin Kleb na kigogo wa zamani wa Shirika
la Umeme Tanzania, TANESCO, Isaac Chanji.
Lakini kuna uvumi kwamba na milionea Yussuf Manji amechukua
fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga,
Francis Kaswahili anaendelea kukataa kwamba amechukua.
Idadi ya waliochukua fomu hadi sasa inafika watu 11, baada
ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa,
John Jambele, Peter Haule, Gaudicius Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah,
wote Ujumbe.
Uchaguzi wa Yanga
unaokuja baada ya Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji iliyoingia madarakani
mwaka juzi, kujiuzulu akiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na
mwisho wa zoezi la kuchukua ni kesho, wakati kurudisha ni kesho saa 10:00 jioni
na usaili ni Juni 19, mwaka huu.Kaswahili amesema kesho ikifika saa 10:01 hatapokea fomu wala kutoa fomu, kwani saa 10:00 ndio mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea wote.
Wanachama wa Yanga wakiwa kwenye mlango kabisa wa kuingia klabuni, kusubiri watu wanaokwenda kuchukua fomu |
No comments:
Post a Comment