BUKOBA
Halmashauri za wilaya mkoani Kagera zimetakiwa kutenga fedha kwa ajili ya
kununua matrekta makubwa ili kuwezesha kuwasaidia wakulima kutumia zana za
kisasa ikiwa pia ni njia ya kutekeleza sera ya kilimo kwanza.
Akitoa taarifa ya hali ya chakula mkoani Kagera mkuu wa mkoa
kagera kanali mstaafu Fabian Masawe amesema kuwa mkoa katika kipindi cha mwaka
2011hadi 2012 zaidi ya hekta laki 6
zililimwa na na matarajio ilikuwa kuvuna
zaidi ya tani millioni moja.
Amesema kuwa kutokana na hali ya mvua zinazoendelea huenda
ikashindika baada ya baadhi ya maeneo kuwa na mvua nyingi na kuhalibu mazao na na hivyo
kushindwa kufikia malengo
Amesema kuwa ikiwa matrekta yatanunuliwa kuna uwezekano wa
kuongeza hekta za kilimo lakini pia kuna uzalishaji utaboleshwa na kusababishwa
kutokomeza umasikini kwa baadhi ya jamii
Wilaya zilizotihtisha kununua matrekta ni pamoja na Ngara,
Biharamulo , Muleba , Bukoba manispaa, karagwe na wilaya ya Bukoba wilaya ya
Misenyi haikoonyesha uwezekano wa kununua trekta hata moja . MWISHO
No comments:
Post a Comment