Sunday, June 17, 2012

Christina Shusho kuwania tuzo ya nyimbo za Injili

Na Mwandishi Wetu

Mwanamuziki wa Injili nchini Christina Shusho ametajwa kuwania tuzo ya mwanamuziki bora wa Kike na mwanamuzi bora wa Afrika Mashariki.
Bi. Shusho ambaye amekuwa akipanda chati kila siku kutokana na nyimbo zake zinazoonesha kupendwa nadani na nje ya nchi anakuwa mwanamuziki wa injili wa kwanza kutoka Tanzania kuwania tuzo hiyo ya Injili.
Shusho amepata nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na watu mbali mbali kutoka ndani na nje kutokana na huduma yake ya nyimbo za injili.
Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa Juli 7, mwaka huu huko London Uingereza ambapo awanawania katika vipengere viwili, cha kwanza Mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki na mwanamuziki bora wa kike  ambapo katika nafasi hiyo wako wanamuziki mangwiji kutoka bara la Afrika.
Chonde chonde Wanzania na wapenzi wa nyimbo za Injili mnaalikwa kumpigia kura kupitia Website ya http://scmgospelawards.com/
Kumbuka mwaka huu Shusho ndiye aliyetutoa kimaso maso ambapo ni nafasi adimu sana kupatikana kwetu.Zingatia kuwa katika nchi ya Kenya imetoa wanamuziki watano wanaowania tuzo hizo, je kwa nini Tanzania tusiweze kwani tunae mwakilishi mmoja tu amnbapo kwa Kenya wao wanao watanao ambao huenda wakagawana kutra hivyo ikawa faifa kwetu.
Kazi kwetu...

No comments:

Post a Comment