Tuesday, June 5, 2012

Sakata ya Ngara, Chato na ofisi yake kupata hati chafu,RC Kagera awashukia wakaguzi wa ndani


Na Theonestina Juma, Bukoba
KUTOKANA na Halmashauri ya wilaya ya Ngara  na Sekretarieti ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kupata hati yenye mashaka Mkuu wa mkoa huo, Kanali Fabian Massawe amewageukia wakaguzi wa hesabu za ndani katika halmashauri za Mkoani hapa kuwa huenda wanakula nao.
Alisema sababu za kusema hivyo inatotokana na mkoa hauwezi kupata hati yenye mashaka wakati wakaguzi wa ndani wapo, na hilo ndilo jukumu lao kubwa ndani ya halmashauri zote za mkoani hapa pamoja na sekretarieti ya ofisi yake.
Kanali Massawe  alisema hayo jana  wakati akifungua  kikao cha Kamati ya Ushauri wa Mkoa  kilichofanyika mjini hapa.
 Alisema kutokana na hali ya Mkaguzi na Mdhibiti  Mkuu wa hesabu ya serikali (CAG) ndiye anayekuja na kubaini madudu yanayotendeka ndani ya halmashauri hizo inaonesha wazi kuwa wakaguzi wa ndani kushindwa kuwajibika katika ukaguzi wao na huenda wamekuwa wakishiriki katika wizi wa fedha za serikali na hali imepelekea baadhi ya wilaya kupata hati chafu.
Alisema CAG katika ukaguzi wa mwaka wa fedha wa 2010 /2011   imeoenekana wilaya za Ngara, Chato na sekretalieti ya mkoa wamepata hati chafu hali ambayo inaonyesha mashaka katika utendaji wao.
Alisema kufikia hatua ya halmashauri hizo kupata hati chafu inatokana na pia na uzembe na ubadhirifu ulikothiri ndani ya halmashauri hizo jambo ambalo halitaendelea kuvumiliwa.
“Siwezi kuendelea kuvumilia madudu kama haya, kwanini makosa haya yasiobainishwe awali na wakuguzi wetu wa ndani badala ya kuja kuvumbuliwa na wageni kutoka nje…. hapa kuna nini?alihoji
“Kabla ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali hajafika ni lazima wakaguzi wa ndani wawe wameishainisha makosa ya matumizi mabaya ya serikali kwani ni aibu makosa ya ndani kuonwa na watu wa nje wakati mhusika mkuu anakuwepo katika eneo hilo”alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo hatua kali zitaanza kuchukuliwa  kwa kuwafukuza kazi  wahusika pindi watakapobainika kabla ya CAG hawajafika na kuwataka wakurugenzi kuwa makini kwa sasa kwani fedha za wananchi zimekuwa zikitumika kwa maslahi binafsi.
Akizungumuzia suala na makusanyo ya mapato katika halmashauri amesema kuwa inasikitisha kwa halmashauri kushindwa kufikia malengo waliyo jiwekea  kwa  ya ukusanyaji wa mapato ambapo ameeleza kuwa hakuna halmashauri iliyovuka asilimia 40.
Kanali Masawe amesema kuwa makusanyo mengi yamekuwa yakiishia midomoni kwa wachache  hasa watumishi wasio waaminifu katika matumizi ya fedha za serikali na kuwaagiza wakuu wa wilaya kuanza na hilo la kutokomeza mchwa katika halmashauri hizo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment