Saturday, June 29, 2013

Rais Kikwete afungua mkutano wa majadiliano ya Smart Parterneship

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana

Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza
Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha
Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni

Maajabu ya tango katika afya ya mwanandamu



 
Hawakukosea wale waliosema  kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako.  Matunda mengi yana manufaa lakini tango tunasema limetia fora.
 Kwanza linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc.
Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.
 Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.
Nne, unataka kuondoa ‘hangover’ au maumivu makali ya kichwa, kula tango ambalo lina sukari ya kutosha na vitamin zitakazoweka mambo sawa mwilini.
 Tano, umechelewa kwenda kwenye usaili, viatu ni vichafu, chukua vipande vya tango na sugulia katika viatu. Vitang’aa.
Sita, umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya  mdomo.
Saba, midomo imekauka na inauma? Chukua kipande cha tango na sugulia mdomoni,  utaona mabadiliko katika midomo.
 Nane, umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane.
 Tisa, umekosea kuandika katika ubao au ukuta, chukua maganda ya tango na usugulie taratibu, wino au rangi hiyo itafutika kabisa.
 Kumi, pia, tango lina uwezo mzuri wa kusafisha vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu au maji ya chumvi.
0
Share




Vituko vya usalifirishaji wa Watumwa enzi hizo alivyoona Obama nchini Senegal

Obamas at the 'Door of No Return': First Family makes emotional trip to former slaving port in Senegal from where captives were shipped to America 

Personally poignant: President Obama said that the visit to the former slave trade hub was important to him as an African American and an African American President tasked with protecting human rights
President Obama said that the visit to the former slave trade hub was important to him as an African American and an African American President tasked with protecting human rights
Tragic tourist destination: The Obamas visited Goree Island's Door of No Return where the slaves would embark on their journeys across the Atlantic Ocean
The Obamas visited Goree Island's Door of No Return where the slaves would embark on their journeys across the Atlantic Ocean
Facing history: President Obama took a tour of Goree Island outside of Dakar, Senegal where slaves used to be depart on boats bound for America in the late 18th century
Facing history: President Obama took a tour of Goree Island outside of Dakar, Senegal where slaves used to be depart on boats bound for America in the late 18th century
Touring: President Obama was accompanied to Goree Island by his wife Michelle, their eldest daughter Malia, Michelle's mother Marian Robinson and their niece Leslie
President Obama was accompanied to Goree Island by his wife Michelle, their eldest daughter Malia, Michelle's mother Marian Robinson and their niece Leslie
Obama peered out at the crashing waves through the island's 'Door of No Return,' at first by himself
Obama peered out at the crashing waves through the island's 'Door of No Return,' at first by himself
Mrs Obama joined him at the poignant doorway, and he said that the visit helped remind them of the importance of protecting civil rights
Grim history: President Obama has a sombre moment at the Door of No Return
President Obama has a sombre moment at the Door of No Return
Meaningful: Though the Maison des Esclaves has become a popular tourist destination, it was one of the more minor slave shipping ports in Senegal

Though the Maison des Esclaves has become a popular tourist destination, it was one of the more minor slave shipping ports in

Maandalizi ya ujio wa Obama Tanzania ni funga kazi

Dar es Salaam. Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huyo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.

 

Wednesday, June 26, 2013

Hali ya Nelson Mandela ni kama Nyerere wingu nzito latanda


Mwanamama akipita katika ukuta wenye picha ya Nelson Mandela mjini Soweto. Mandela anapatiwa matibabu huko Pretoria na hali yake inaelezwa kuwa ni mahututi na wananchi wamekuwa wakimwombea nafuu ya haraka. Picha ya AFP  

 Habari zilizotapakaa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Johannesburg ni kwamba hakuna matumaini ya Mandela kupona na sasa familia yake inajadiliana kuhusu taratibu za mazishi yake huku mwenyewe akiendelea kupumua kwa msaada mashine hospitalini alikolazwa.
Mandela (94) amelazwa katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo, Med – Clinic, Pretoria kwa siku ya 19 sasa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Ikulu ya Afrika Kusini tangu Jumapili, usiku zinathibitisha kwamba hali yake ni mahututi.
“Tunasubiri habari mbaya za kifo cha Mandela maana taarifa zinazotolewa na Serikali kuhusu hali ya afya yake ni dalili kwamba hawezi kuishi tena,” alisema mkazi wa Johannesburg, Doroth Nyathi alipozungumza na mwandishi wetu na kuongeza:
“Watu wanaamini kwamba Mandela ameshafariki dunia, lakini Serikali na familia yake wanatuficha tu, labda wanasubiri maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mwezi ujao.”
Mandela anafikisha umri wa miaka 95 Julai 18 mwaka huu, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda asiifikie siku hiyo ambayo ni maarufu kama “Mandela Day” kutokana na kuzorota kwa afya yake.
“Kama mtu hajafa mnawezaje kukaa kujadili mahali pa kumzika, ndiyo maana nimekwambia ni dhahiri kwamba Mzee Madiba (Mandela) tayari amefariki, ila wanatuficha tu,” alisema Nyathi.
Nyathi alikuwa akirejea taarifa za vyombo vya habari kwamba familia ya Mzee Mandela ilikutana katika kikao cha siri juzi kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 08:00 mchana kujadili “mahali pa maziko” ya shujaa huyo aliyeongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, kufungwa jela miaka 27 na baadaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Habari kutoka katika kikao hicho kilichohudhuriwa na waziri katika Serikali ya Afrika Kusini ambaye pia ni mwanafamilia wa Mandela na mmoja wa viongozi wa vyama vya siasa, zinasema baadhi walikuwa wakitaka azikwe alikozaliwa huko Mvezo, wakati wengine wakitaka azikwe Qunu.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimesema Mandela atazikwa Qunu, taarifa ambazo hata hivyo, hazijathibitishwa na Serikali ya Afrika Kusini ambayo imekuwa ikisisitiza kwamba “Familia ya Mandela isaidiwe katika kipindi hiki kigumu.”
Kwa upande wake, mkazi wa Pretoria, Lisa Wright alisema wasingependa kumpoteza Mandela lakini kwa jinsi hali inavyoendelea ni dhahiri kwamba maradhi yanamzidi nguvu hasa kutokana na umri mkubwa.
“Tutamkumbuka sana Mzee Mandela, amechangia kufuta uhasama baina ya watu weupe na weusi hasa kutokana na moyo wake wa kusamehe baada ya kutoka gerezani, hivi leo suala siasa za ubaguzi litageuka historia hasa baada ya kizazi hiki kupita,” alisema Lisa.
Nyumbani kwa Mandela, eneo la Houghton, Mtaa wa Laan 12 jijini Johannesburg, watu kwa makundi wamekuwa wakifika na kuweka maua kwenye vitalu vinavyozunguka makazi yake na wengine wakiandakia ujumbe wa kumtakia heri ya kupona haraka kwenye mawe madogomadogo yaliyoko kwenye vitalu hivyo.
Makazi hayo pia yamezungukwa na magari yanayotumiwa na waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali, ambao kwa zaidi ya wiki tatu wameweka kambi katika eneo hilo tangu kuripotiwa kuzorota kwa afya ya kiongozi huyo.

Hali ya mzee Nelson Mandela ni tete

Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.

Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40.

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.

Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo."
Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj.

Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu alipopokelewa hospitalini hapo.
 
Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994, alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria mapema Juni 8 kufuatia maambukizi kwenye mapafu.
Ilidaiwa jana kwamba Mandela hajitingishi na familia yake sasa inajadili uwezekano wa kusitisha matibabu.

Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili akipambana na maambukizi hayo, lakini taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya ya Mandela inaimarika.

Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka hadi asilimia 50 na hakufungua macho yake kwa siku kadhaa.
 
Pia alitakiwa kufanyiwa oparesheni mbili hivi karibuni, moja kutibu vidomda vya tumbo zilivyokuwa vikichuruzika damu na nyingine kuchomeka mpira mwilini mwake, imeripotiwa.
Taarifa hizi zinaashiria kwamba suala la Mandela ni kubwa kuliko inavyoripotiwa na mamlaka za Afrika Kusini.

Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town. Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.

Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne tangu Desemba, tangu mwaka jana.
  

Mfalme wa Mswati II atua nchini

03Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya  kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smat Patnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu. Picha na OMR
04Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya  kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smat Patnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu. Picha na OMR
05Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ‘Smat Patnership’, unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati. Picha na OMR