Na
Theonestina Juma, Bukoba
JESHI la
polisi Mkoani Kagera limefanikiwa kuua jambazi mmoja na kukutwa na silaha kali
za kivita zikiwemo bunduki tatu, risasi 246 mabomu matatu ya kurushwa kwa mkono
wakiwa katika harakati za kutaka kuvamia mgodi wa Tulawaka wilani Biharamulo.
Hayo
yamebainishwa na Kamanda wa polisi Mkoani Kagera, Philip Kalangi
wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo asubuhi na kwamba tukio hilo lilitokea Juni 9,m mwaka huu saa 10.30 alafajiri Mavota Tulawaka wilayani humo.
Kamanda
Kalangi alisema jambazi huyo aliuawa baada ya polisi kupambana na kundi la
majambazi wasiojulikana idadi kwa dakika kadhaa, ambao walizidiwa nguvu na mmoja kuuawa na
wengine kukimbilia kusikojulikana.
Alisema
baada ya jambazi huyo kuuawa alipopekuliwa alikutwa na silaha hizo, zikiwemo
bunduki tatu aina ya AK 47 mbili zikiwa na namba UC 55231990,UC 16081998 na pamoja
na bunduki aina ya Short gun mashine (SMG) yenye namba 56128033262 ambapo mbili
zikikuwemo kwenye mfuko wa kiroba ambayo alikuwa akiitumia katika kujihami katika tukio hilo.
Alisema
mbali na kukutwa na silaha hizo pia alikutwa na sare pea mbili ambazo
zinafanana na za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) buti jozi moja koti ya mvua
ambazo zilikuwwa zimefungiwa bunduki mbili na magazine saba zilizokuwa na
risasi.
Alisema
mwili wa jambo huyo umehifadhiwa katika hospitali Teule ya Wilaya ya
Biharamulo ambapo msako unaendelea wa
kuwatafuta majambazi wengine waliokimbia kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment