MAREHEMU WILLY EDWARD
Yasema ni pigo kubwa kwa wadau wa
habari
·
Yawataka wanahabari
kumuenzi
Kampuni ya simu ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mwanahabari
mahiri Bw. Willy Ogunde Edward kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki
hii.
“Tunatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu, waajiri
wake na kipekee familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na mpiganaji na
kamanda wetu aliyekuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari
nchini.”Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza
Marehemu Willy Edward alikuwa ni mdau wa habari mwenye
msaada na ushauri pale anapohitajika na aliiwakilisha vyema tasnia hii ya habari
tangu alipokuwa Majira mpaka kabla umauti haujamkuta akiwa Mhariri wa habari wa
Jambo Leo.
Marehemuatakumbukwa kwa jinsi ambavyo alikua mahiri
katika kazi yake, ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kwamba mchango wake
utaendelea kuwa chachu hasa kwa vizazi vijavyo vya wanahabari chipukizi
nchini.
“Tutamkumbuka sana Marehemu Willy ambae alikuwa ni mpole
na mcheshi na mwenye utashi wa mafanikio katika kazi zake. Hakusita kutoa
ushauri kuboresha uandishi wa habari ili kutoa ujumbe uliokamilika na sahihi
pale alipoona mapungufu kutika habari husika”. Alisema Meza.
Mkurugenzi huyo Mkuu wa Vodacom amesema kampuni yake
daima ina thamini na kuheshimu mchango wa wanahabari katika maendeleo ya taifa
na uimarishaji ustawi wa jamii na kuamini kuwa wanahabari waliobaki wataendeleza
urithi (Legacy) aliouacha marehemu Willy.
Mungu azilaze roho za Marehemu BwWilly Ogunde Edward
mahali pema peponi –Amen.
No comments:
Post a Comment