Prof. Ibrahim Lipumba kushoto Mwenyekiti wa chama cha
wananchi CUF, Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, na Mwenyekiti
mtendaji wa makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi wakijumuika pamoja na viongozi
wengine, ndugu jamaa na marafiki pamoja na waombolezaji wengine waliohudhuria
katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Willy Edward Ogunde aliyekuwa mhariri
mkuu wa Gazeti la Jambo leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam
jana.
Mwili wa marehemu Willy Edward Ogunde aliyekuwa mhariri
mkuu wa Gazeti la Jambo leo ukiwasili katika viwanja vya mnazi mmoja jijini
Dar es salaam jana.
|
Mjane wa
Marehemu Willy Edward Bi Rehema akifarijiwa na ndugu huku akilia kwa uchungu kwa
kumpoteza mume wake mpendwa marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti wa
IPP Reginald Abraham Mengi, Akimfariji Athumani Hamisi katika msiba
huo
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP
Reginald Abraham Mengi, Akitoa heshima zake za mwisho
kwa mwili wa marehemu Willy Edward wanaofuatia nyuma yake ni Mwenyekiti wa CUF
Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape
Nnauye
Baadhi ya waombolezaji
waliohudhuri katika kuuaga mwili wa marehemu Willy Edward wakiwa katika mstari
tayari kwa kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
No comments:
Post a Comment