Tuesday, June 5, 2012

Viongozi anzisheni mashamba darasa wananchi waige kutoka kwenu

Theonestina Juma,Bukoba

MKUU wa Mkoa Kagera,Kanali Fabian Massawe
amewahimiza viongozi wote wa mkoani hapa kuwa na mashamba darasa kwa
ijili ya kuonesha mifano na kuwezesha wananchi kuiga kutoka
kwao.

Kanali Massawe amesema hayo jana (leo) wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri wa Mkoa Kagera (RCC) kilichofanyika mjini hapa na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo

Alisema " hatuwezi kila mara tunapanda majukwaani kuimba kilimo kwanza bila vitendo, hivyo ni
wajibu wetu kuwa na mashamba ya mifano ili wananchi waige kutoka
kwetu".

 Alisema kwa wale viongozi ambao hawana mashamba ya kulima heri
waelekee wilaya ya missenyi watapewa sehemu ya kilimo.

"Kwa wale ambao hawana maeneo ya kulima nendeni kwa Mkuu wa wilaya ya Missenyi  Kanali
Issa Njiku atawapeni, pia bado kuna maeneo makubwa ya wazi yatumieni
katika kilimo cha mifano"alisema.

 Aidha aliwataka viongozi hao kuwahimiza wananchi kuendesha kilimo cha utaalam ili kuongeza tija na
biashara kwa wananchi.

Halikadhali wanatakiwa kuwasaidia wakulima wadogo kuboresha kilimo chao ikiwa na pamoja kukopa matreka madogo kwa ajili ya kilimo

Pia kila halmashauri zinatakiwa kuunda vikundi vya vijana ili kuweza kuendesha kilimo cha kisasa kwa kutumia matrekta kutokana na kwa sasa kilimo cha mkono ni changamoto kubwa kwa vijana
wa kizazi hiki.
mwisho

No comments:

Post a Comment