Monday, June 25, 2012

Sakata la mila potofu ya wanaume wa kihaya kupakuliwa chakula kingi na kula peke yao bila watoto, waanza kupewa elimu

Bukoba
WAKATI katika familia nyingi hujizatiti kwa kuhakikisha kuwa watoto ndiyo wanakula chakula bora ili kuwa na afya, hali iko tofauti kwa asilimia kubwa ya wanaume wa kabila la Wahaya ambao wakati wa kula wao ndiyo hupakuliwa chakula kingi.
Kama hilo halitoshi, wanaume hao wanapopewa chakula hicho  hupenda kula peke yao bila watoto wao, ambao wao huishia kula chakula kidogo kama ni ndizi basi mboga ni kiduchu mchuzi mwingi.
Kutokana na hali hiyo ambayo imeelezwa kushamiri na kuzoeleka katika kata ya Kasharu katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba, uongozi wa kata hiyo juzi ulilazimika kuitisha mkutano wa dharura uliolenga kutoa elimu kwa wanaume kuachana na huo mfumo dume.
Hata hivyo, tabia hii si kwamba iko huko Kasharu pekee, hata kwa baadhi ya wanaume walioko katika Manispaa ya Bukoba, hupendelea kula vinono peke yao huku watoto wao wakibaki kushindana kuwavizia wamalizapo tu kula hukimbilia  mezani kuondoa vyombo lakini lengo kubwa likiwa ni kutaka kuonja makombo yaliobaki.
Pamoja na hayo, lawama huenda wakatupiwa wake zao ambao nao wanakubaliana na huo mfumo dume, kwani ndiyo wanaowaandalia vyakula hivyo, huku watoto wakiwaachia chakula kiduchu mchuzi NDI!.
Wanawake wa kabila hilo nadhani wao wanaojukumu kubwa, la kuhakikisha kuwa wanakutanisha meza moja waume zao pamoja na watoto hao, na si watoto wanaachwa kula mchuzi kwa ndizi ama wali huku baba yao akipakuliwa vinono tena chakula kingi kuzidi watoto.
KAAAAAAAAAAAZI  KWEEEEEEEEEELI KWEEEEEEEEEEEEELI NSHOMILE.

No comments:

Post a Comment