Thursday, January 31, 2013

10 Wahofiwa kufa maji Zanzibar


Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso 

Zanzibar
BOTI ya abiria iliyokuwa ikitokea Pangani mkoani Tanga kwenda Zanzibar ikiwa na watu 32 juzi usiku ilizama katika eneo la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Zanzibar ambapo watu 10 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha.

Taaarifa zilizofikia gazeti hili jana jioni zilisema kati ya abiria 27 na wafanyakazi watano waliokuwa kwenye boti hiyo, ni watu 20 tu waliokuwa wameokolewa wakati wengine 10 wakiwa hawajulikani walipo.

Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso alisema jahazi liitwalo Sunrise liliondoka Tanga juzi saa 2:00 usiku kuelekea Zanzibar, lakini lilipigwa na dhoruba katika eneo la Nungwi.

“Mpaka sasa watu 22 wameokolewa akiwamo nahodha Abdallah Selemani, kumi wanatafutwa ijapokuwa wanahofiwa kuwa wameishakufa. Kati ya hao ni watoto watatu na watu wazima ni saba,”alisema Senso katika ujumbe alioutuma kupitia simu yake ya mkononi.

Aliendelea: “Boti kutoka Tanga ipo kwenye eneo la tukio kusaidia uokozi na wakazi wa Kaskazini Unguja wamepokea watu waliookolewa na kuwapa huduma. Taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia Tanga na Zanzibar”.

Hata hivyo idadi ya watu waliookolewa kwa mujibu wa Senso ilitofautiana na ile iliyokuwa imetolewa awali na Kamanda wa Wanamaji na Bandarini Zanzibar, SP Martin Lisu aliyesema juhudi za kuwaokoa abiria hao zilikuwa zikiendelea na kwamba waliokuwa wamepatikana wakiwa hai ni watu 21.

Lisu alisema abiria hao walionusurika kifo walipelekwa hospitalini kwa ajili ya kuchunguzwa afya zao na wengine walipatiwa huduma za kwanza kutokana na mshtuko walioupata.

“Kusema kweli tulifanikuwa kuwaokoa abiria 21 na wengine siwezi kusema kama wamezama ila nachoweza kusema ni kwamba bado hatujawapata,” alisema Kamanda Lisu na kuongeza:
“Taarifa nilizonazo ni kwamba, hii boti ilikuwa ikitokea Pangani, ilipofika eneo la Nungwi ikakubwa na dhoruba kali na kisha kuanza kupoteza mwelekeo”.

Eneo la Nungwi
Eneo la Nugwi lina historia ya kusababisha ajali za mara kwa mara na mara ya mwisho ndiko ilitokea ajali ya meli ya MV Spice Islander iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400 mwaka 2011.

Ajali hiyo ilielezwa kusababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji ikiwemo kukosekana kwa ukaguzi kabla ya meli hiyo kuondoka.Taarifa zilizema kuwa meli hiyo ilizidisha idadi ya abiria na mizigo hivyo ilipofika eneo la Nungwi ilizidiwa na kuanza kuzama.

Katika kujaribu kusaka ukweli wa mambo, Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein aliunda tume maalumu kuchunguza mazingira yaliyosababisha ajili hiyo.
Ripoti ya tume hiyo ilifichua uzembe uliojitokeza kwenye mamlaka husika na kupendekeza hatua kadhaa ili kuimarisha hali ya usafiri kwenye maji.

Ajali nyingine kubwa ni ya meli ya MV Skagit iliyotokea mwaka jana ikiwa inakaribia katika bandari ya Zanzibar, ambayo hatua za awali za uokoaji zilishindikana na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Ni kipindi kirefu hatujapata wala kumuona sangara mkubwa kiasi hiki

 Baadhi ya wafanyabishara wa soko kuu la Muleba mjini wakishangaa kumuona samaki aina ya sangara mwnye kilo zaidi ya 40 akiwa ameletwa sokoni humo kwa ajili ya kuuzwa.Mwenye samaki huyo,  Bw.Deocres John mwenye kofia kichwani alisema ni miaka mingi hajawahi kupata samaki kama huyo ambapo samaki huyo alikuwa akiuzwa sh. 100,000 baada ya kuondolewa bon do lake lililokuwa na uzito wa nusu kilo ambalo huuzwa sh. 40,000.

Tuwafundishe watoto wetu kufanya kazi za ndani



 Mtoto umuleavyo ndivyo akuaaji , hapa mtoto Rainer Jeremia miaka 5 akimsaidia mama yake kufuta vyombo baada ya kuviosha.

Wednesday, January 30, 2013

Lulu Karibu uraiani na uwe makini kwa kila jambo

 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililompeleka Mahakama Kuu kukamilisha taratibu za kupata dhamana.
Lulu akiingia Mahakamani
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyuma akifuatiwa na mama yake mzazi.
Lulu akiondoka mahakama hapo.

Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. 
Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kuwasilisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa Msajili wa Mahakama kila mwezi. 

Tuesday, January 29, 2013

Leo Babu yetu mzee Aloyce Amworo ametimiza mwaka 1 tangu Mungu amwite

TAREHE kama hii ya leo, Januari 29, mwaka 2012 siku ya jumapili, ni siku ambayo babu yetu kipenzi alitutoka, katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza. Kwa leo Babu yetu MZEE ALYOCE AMWORO ametimiza mwaka mmoja tangu atutoke.Babu yetu unakumbukwa na mkeo Lucia Amworo, wanao Mary, Odira, Hadhrian, Norbart na Benedict.Pia unakumbukwa na wajukuu zako Theonestina Juma, Euphrasia, leonida, Hilda, Happiness, Beatha, Alyoce1, Editha, Alyoce 2,Aloyce3,Aloyce 4, Makori, Judith , Joseph, Luciana pamoja na vitukuu wao , ndugu, jamaa na marafiki.
Misa ya kumwombea marehemu inafanyika leo katika kijijini kwake Randa Wilaya ya Rorya ambapo inaendeshwa na Padri wa Parokia ya Ingri Romanus Ciupaka.Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe .AMENA.

Saturday, January 26, 2013

Hivi kuendesha baiskeli huku umevaa suti inalipa kwa karne hii?

tweet~ spons~~ by @[480824948595792:274:LeO_MedIa_Blogspot] kumbukumbu
Harakati za Tanzania kudai Uhuru, hayati Mwalimu Julius Nyerere alitumia baiskeli kutafuta uhuru, huku akiwa amevaa suti.Hivi kwa sasa ni nani anaweza kufanya hivyo?

Friday, January 25, 2013

Majambazi wateka magari 5 likiwemo na la wanajeshi wa Rwanda, wapora abiria mamilioni ya fedha Biharamulo

Na Theonestina Juma, Kagera
 ZAIDI ya majambazi 10 wakiwa na bunduki takriban tisa wameteka magari matano likiwemo  lilikodiwa na wanajeshi 10 wa nchini Rwanda waliokuwa wakienda Jijini Dar Es Salaam kununua magari na wameporwa mamilioni ya fedha pamoja na abiria wengine wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini Bukoba, na kuthibitishwa na diwani wa kata ya Rusahunga Bw.Amon Mizengo na kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Phillip Kalangi tukio hilo limetokea Januari 24, mwaka huu saa 12.00 asubuhi katika kijiji cha Kikoma barabara ya Biharamulo -Rusumo katika eneo la mizani ya Nyakahura wilayani humo.
Jumla ya fedha walizoporwa abiria hao pamoja na wanajeshi ni milioni 4.2 za Kitanzania, Dola 175,000, Faranga za Rwanda 85,500 pamoja na simu za mkononi.
Habari hizo zinadai kuwa magari yaliotekwa yalikuwa yamewabeba wafanyabiara waliokuwa wakienda katika mnada wa ng’ombe wa Rusahunga wilayani humo.
Aidha gari lingine ni aina ya hiace lililokuwa limebeba wanajeshi 10 wa nchini Rwanda waliokuwa wakienda katika bandari la jijini Dar Es Salaam kwa shughuli la kununua magari kulingana na hati zao sa kusafiria ambapo  walikuwa wamevaa kiraia tu.  
Hata hivyo haijajulikana kama walikuwa wakienda Jijini Dar Es Salaama kwa shughuli za kiserikali ama zao binafsi.
Pia magari mengine ni yale  yaliokuwa yakienda nchi jirani ya Rwanda,
 huku mengine yakitoka Ngara kwenda Kahama mkoani Shinyanga .
Hata hivyo magari hayo ambayo namba zao za usajili hazijajulikana,wala wamiliki wao na idadi ya abiria waliokuwemo, inaelezwa kuwa walipofika eneo hilo majambazi hao walikuwa wakiwasimamisha kwa kuwanyonyeshea bunduki.
"Hakuna mawe wala magogo yaliokuwa yamepangwa barabarani,majambazi hao walikuwa wakiwaonyooshea bunduki tu madereva hao na wao wanasimamisha, hakuna waliojeruhiwa katika tukio hilo"alisema Bw.Mizengo licha ya habari zaidi kueleza kuwa majambazi hayo yalikuwa yamepanga mawe na magogo barabarani.
Habari zaidi zina sema kabla ya kutekeleza azima yao walifyatua risasi kadhaa hewani.
Katika utekaji huo, majambazi hayo wamewapora abiria mali zao zote waliokuwa nazo na kisha kutokomea kusiko julikana.Hata hivyo majambazi hao wanasadikiwa kuwa ni wa kutoka nchi jirani ya Burundi kutokana na lugha ya Kirundi waliokuwa wakizungumza wakati wa tukio hilo.
Bw. Mizengo alisema kuwa katika tukio hilo limempata na Askari polisi mmoja wa kituo cha Nyakahura  ambaye jina lake halijapatikana aliyekuwa anaenda Kahama Mkoani Shinyanga.

N

Wednesday, January 23, 2013

Baba amuua binti yake wa mwezi mmoja tu kisa mkewe amemchosha kwa kumzalia watoto wa kike pekee



Na Theonestina Juma, Kagera
MKAZI  mmoja wa wilayani Ngara mkoani Kagera anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma ya kumuua mwanae wa kike mwenye umri wa  mwezi mmoja kwa madai kuwa  mkewe amemchosha kumzalia watoto wa kike pekee .
Mtu huyo anayedaiwa kushilikiwa na jeshi hilo ametambuliwa kuwa ni Bw. Kahungu ambapo tukio hilo limetokea Januari 19 mwaka huu wilayani humo.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa polisi mkoani hapa, Bw. Phillip Kalangi, kwa kipindi kirefu, Bw. Kahungu alikuwa akimtuhumu mkewe   Bi. Vanencia kumzalia watoto wa kike pekee.
“Katika uchunguzi wa awali wa Jeshi la polisi ubaini kuwepo kutoelewana katgi ya wanandoa hao, mke na mume ambapo  Bw. Kahungu  alikuwa akituhumu mkewe kumzalia watoto wa kike pekee wakati yeye anataka wa kiume”alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, wakati mkewe akiwa mjamzito yeye alikuwa na mategemeo makubwa kuwa mkewe atamzalia mtoto wa kiume.
Hata hivyo, bila kutarajiwa baada ya mkewe kujifungua mtoto wa kike na kupita takribani mwezi mmoja, Bw. Kahungu alimuua mtoto huyo ambaye jina lake halijajulikana kwa kumnyonga shingo.
Bw. Kahungu anatarajiwa kufikishwa ,mahakamani wakati wowote ,mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.
mwisho

Saturday, January 19, 2013

Hii kali simu zinapopangwa barabarani kama nyanya nchini China

WAPENDWA WATANZANIA WENZANGU, HII PICHA NI HALI HALISI HUKO CHINA SIMU ZINAUZWA BARABARANI, ZIKIWA ZIMEPANGWA KAMA NYANYA SOKONI..
Kweli duniani kuna mambo kama ndiyo kukua kwa teknolojia, simu sasa zinapangwa barabarani kuuzwa kama nyanaya hakuna kulala

Friday, January 18, 2013

Jamani mapenzi... mume atenganisha kichwa na kiwili wili cha mkewe naye ajimaliza kwa kujitia kitanzi... kisa wivu


Na Theonestina Juma, Kagera

MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Kikuku kata Kagoma wilayani Muleba, Bi. Bilivu Festo (40) ameuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na kisha kutenganishwa kichwa na kiwili wili chake na mume Bw. Festo Kibenderena (56) na kisha kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni  kutokana na wivu wa mapenzi.
Tukio hilo la aina yake ambalo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoa Kagera, Pillip Kalangi limetokea Januari 16, mwaka huu saa 12 jioni katika kijiji cha Kikuku kata ya Kagoma wilayani Muleba.
Chanzo cha mauji hayo ya kikatili kimeelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi ambapo, Bw. Festo alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa anasaliti ndoa yao kwa anatembea nje na wanaume wengine.
Wanandoa hao ambao wameacha watoto wanne, siku ya tukio, baba yao aliwatoa nyumbani kwenda kupalilia njugu shambani ambapo kumbe alikuwa na lengo lake la kutaka kumuua mkewe.
Katika tukiko hilo ambalo wakati likitokea, mtu wa kwanza kutoa taarifa  ya mauaji hayo ni mtoto mdogo wa miaka mitatu ambaye ni mwanaye Bw. Godwin Kasebano anayemwita Bw. Festo kuwa baba mdogo wake.
Imeelezwa kuwa siku hiyo ya tukio, mtoto huyo ambaye jina lake halijapatikana alienda kwa baba yake na kumwelezea jambo kwa ishara ambapo Bw. Godwin alienda kwa baba yake mdogo huyo na kukuta Bi.Bilivu akiwa ameuawa kwa kucharangwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili na kutenganishwa kichwa na kiwiwili huku baba yake mdogo huyo akiwa ametoweka nyumbani hapo.
Hata hivyo, baada ya mauaji hayo, watu walianza kumsaka Bw. Festo bila mafaniko hadi  kesho yake Januari 17, mwaka huu  saa 7 mchana baada ya maziko ya mkewe ndipo aligundulika kuwa amejinyonga.
Mwili wa Bw. Festo  ulikutwa juu ya mti wa mwembe ukiwa unaning’inia akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila  ng’ambo wa pili na watu waliokuwa wakipelekea nguruwe chakula.
Mwili wa Bw. Festo pia ulizikwa siku hiyo ambayo alizikwa mkewe Bi. Bilivu.

Wednesday, January 16, 2013

Majambazi matatu wauawa Muleba katika majibizano ya risasi na polisi



Na Mwandishi wetu
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na jeshi la polisi mkoani Kagera katika majimbizano ya risasi wakati wakiwa katika harakati  za  kutaka kuvamia kituo cha mafuta  wilayani Muleba.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Phillip Kalangi alisema tukio hilo limetokea Januari 14, mwaka huu saa 2 usiku katika kituo cha mafuta cha BP Wilayani Muleba.
Katika tukio hilo kundi la watu wapatao watano walitakiwa kusimama na askari lakini walikataa kutii agizo hilo na hivyo kuanza kuwarushia polisi risasi za moto na polisi kujibu mapigo yao ambapo polisi walifanikiwa kuwauawa watu watatu papo hapo.
Katika jaribio hilo Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwapokonya majambazi  bomu moja la kutupwa kwa mkono,  magobore  mawili , bunduki moja aina ya SMG yenye namba 08462289 na risasi  25.
Aidha kamanda Kalangi alisema miongoni mwa watu hao watano watu wawili walifanikiwa kutoroka kusiko julikana.
 Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wilayani humo  waliopanga kuvamia kituo cha mafuta cha BP na hivyo jeshi hilo kuweka mitego yake.
Alisema kati ya watu hao waliouawa ni mtu mmoja tu ndiye ameweza kutambuliwa kwa jina  Jafety Mwigabo  raia Kirundo nchini  Burundi kulingana na kitambulisho alichokutwa nacho.
Kamanda Kalangi alisema majambazi hao waliouawa  ni miongoni wanaounda mtandao wa majambazi  wanaopora wavuvi mali zao katika ziwa Victoria na kwamba walikuwa wakitafutwa kwa kipindi kirefu na jeshi hilo.
Miili ya majambazi hayo yamehifadhiwa katika kituo cha afya cha Kaigara wilayani Muleba yakisubiri ndugu na jamaa kutambua.
Mwisho.