Martha Mwaipaja akiwa katika huduma. |
Nyimbo zilizomo katika album hiyo itakayobebwa na wimbo ''Ombi langu kwa Mungu''ni pamoja na Jaribu kwa mtu, Adui wa mtu, Yesu ni mzuri, Kweli nimetambua, Kaa namimi tena, Nani ajuaye maumivu, pamoja na Sifa zivume huku wimbo mmoja wa Kaa namimi tena akiwa amemshirikisha mtangazaji wa Wapo Radio Fm ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya New Jerusalem kutoka EAGT Mito ya baraka kijana Silas Mbise.
Akizungumzia zaidi kuhusu album yake hiyo mwimbaji huyo ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na mchungaji John Said, amesema anamshukuru Mungu kwani tayari kila anapoenda kwenye huduma watu tayari wamekuwa wakibarikiwa na kukutana na Mungu kupitia nyimbo hizo mpya kama ilivyokuwa kwa album yake ya kwanza iitwayo ''Kwa msaada wa Mungu'' ambayo inanyimbo zinazobariki wengi mpaka leo pia akakiri kwamba imempatia mafanikio mengi sana kiroho na kimwili kiasi kwamba hawezi kueleza yote.
Amesema anampango wa kufanya tamasha kubwa mwezi wa saba kama mambo yatakwenda sawa kama alivyopanga lakini Mungu ndio mwamuzi zaidi na kueleza kwamba anatarajia kuachia video ya album hiyo mwezi wa nane mwaka huu, maombi yake makuu kwa wapenda uimbaji na huduma yake watambue yakwamba anawapenda sana ni maombi yake kwamba Mungu akakutane na haja za mioyo yao kupitia huduma yake.
Martha Mwaipaja na mumewe mchungaji John Said. |
No comments:
Post a Comment