Na Theonestina Juma, Bukoba
WAFANYABIASHARA wawili wa kijiji cha Izimbya tarafa ya
Rubale katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, wamevamiwa nyumbani kwao na
majambazi sita wenye silaha na kuwapora fedha taslimu zaidi ya milioni 9 na
vitu mbali mbali.
Hayo yamebainishwa jana (leo) na Kamanda wa polisi Mkoani
Kagera, Phillip Kalangi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake.
Kamanda Kalangi majambazi hayo yaliwavamiwa wafanyabiashara Juni 25, mwaka huu saa 2. Usiku ambapo baada
ya tukio hilo walifyatua risasi mbili hewani na kutokomea kusiko julikana.
Aliwataja wafanyabishara hao waliovamiwa na majambazi hayo
kuwa ni pamoja na Philmon Jonathan (35) ambaye aliporwa shi. Milioni 7,848,000
na kisha kwenda kwake Bw. Severine Selestine
ambaye naye walimpora sh. milioni 2 na vitu mbali mbali ambavyo thamani
yake bado havijajulikana.
Katika tukio hilo, majambazi hayo yalimjeruhi mke wa
Selestine Bi. Avodia Severine sehemu ya jicho na mguu kwa kutumia ubao ambapo hali yake imeelezwa
kuendelea vizuri.
Hakuna mtu nayeshikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa
kuhusika katika tukio hilo, ambapo polisi wanaendelea na uchunguzi wao juu ya
tukio hilo.
Katika tukio linguine wahamiaji haramu wapatao 27
wamekamatwa wakiwa wanaishi nchini bila kufuata utaratibu wa nchi.
Wahamaji watatu walikamatwa katika wilaya ya Biharamulo na
wengine 24 walikmatwa katika wilaya ya Ngara, katika msako maalum unaofanywa na
Jeshi la polisi Mkoani hapa kwa kushirikiana na Idara ya uhamiaji.
Wahamaji hao wote walifikishwa mahakamani ambapo baadhi yao
tayari wamesharejeshwa makwao.Msako huo ulianza Juni 6 mwaka huu katika mkoa
mzima ambapo hadi sasa bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment