Baadhi ya vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na mwalimu Siyato kwenye kituo chake.
Haya ni misokoto ya bhangi yakiwa yameshaandaliwa tayari kwa watumiaji.
Baadhi ya vifaa vilivyookotwa na polisi katika barabara ya Uganda mjini hapa vikiwa vimetekelezwa, pamoja na vifaa vya mwalimu.
Gobole linalotumika katika muhalifu wilayani Muleba.
Bukoba
MWALIMU mmoja wa shule ya sekondari ya Nyakato mkoani
Kagera, Bw.Alfred Sitayo (32) amekamatwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuiba
vifaa vya shule vikiwemo vinavyotumika katika maabara ya shule hiyo.
Mwalimu huyo alitiwa mbaroni leo saa 8:00 mchana katika eneo
la barabara ya Uganda katika Manispaa ya Bukoba akiwa naye amefungua kituo cha
kufundisha masomo ya ziada maarufu kama (tuition) katika eneo la Kibeta mjini hapa huku akitumia
vifaa hivyo vya shule alivyoiviiba wakati akiwa mtumishi hapo.
Baadhi ya vitu alivyokutwa navyo mwalimu huyo, ni pamoja na
vitabu mbali mbali, kemikali za maabara ya kemia na viti vya shule hiyo.
Mwalimu huyo aliwahi kuwa kufundisha katika shule hiyo
upande wa maabara ya kemia na kwamba alipoacha kazi hakuweza kukabidhi maabara
ya kemia pamoja na vifaa vyake kwa uongozi wa shule.
Mwalimu huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote
kujibu tuhuma zinazomkabili ya kuiibia serikali akiwa mtumishi wake kinyume na
kanuni, sheria na utaratibu wa mtumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment