Taifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa
tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi
Nyandugu.
Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu
Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto
ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo
Tanzania itakuwa saa 10 kamili.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya
mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo
itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna
mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya
Jumapili.
No comments:
Post a Comment