Msanii mahiri wa HIP HOP
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
'Mr II' a.k.a Sugu, juzi alizikonga nyoyo za mashabiki
wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem
jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la
Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Katika picha juu Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Sugu na Mkoloni wakizidi kuwadatisha mashabiki.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.
Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live.
Nyomi iliyohudhuria Usiku wa Sugu.
Baadhi ya mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sugu.
No comments:
Post a Comment