Na
Theonestina Juma, Bukoba
NISHATI ya
mafuta ya taa imeadimika kwa kipindi cha wiki tatu sasa katika Manispaa ya Bukoba
hali inayopelekea wakazi mji huo kutaabika kila kona kutafuta nishati hiyo.
Hayo
yamebainika katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili mjini hapa takribani
wiki moja sasa ambapo katika vituo takribani sita vinavyouza nishati hiyo vimekaukiwa kabisa.
Uchunguzi
huo umebaini kutukuwepo kabisa kwa nishati hiyo katika Manispaa ya Bukoba,
ambapo gazeti hili lilishuhudiwa baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba
wanaotumia nishati hiyo wakizunguka kila kituo cha mafuta bila mafanikio.
Mmoja wa
wauzaji wa mafuta katika kituo cha Gapco mjini hapa ambaye hakuwa tayari kutaja
jina lake alidai kuwa tatizo la kutopatikana kabisa kwa nishati hiyo, ni
kuadimika Jijini Dar Es Salaam ambapo wanadai kuwa wahusika wagoma kuyatoa.
Halidhakila
muuzaji mwingi katika kituo cha mafuta cha Kanoni Filling Station ambaye naye
alikataa kutaja jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa kituo hicho alisema kuwa
katika kituo hicho hii ni wiki ya pili hawana nishati hiyo.
“Hapa kwetu hii
ni wiki ya pili, hatuna kabisa nishati hiyo, hata sababu ya kuadimika kwa
mafuta hayo mimi sijui, lakini tunamategemeo kuwa huenda yakaanza kuingia kesho
yaani Jumanne wiki hii”alisema muuzaji huyo ambaye ni mwanamke.
Pamoja na
nishati hiyo kuadimika kabisa mjini hapa, lakini katika vituo hivyo vimebandikwa
bei ya lita ya mafuta ambayo ni kati ya sh. 2280 hadi 2283.
No comments:
Post a Comment