Monday, June 18, 2012

Hatima ya nishati ya mafuta ya taa kupatikana Bukoba haieleweki, wananchi wazidi kutaabika

Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Licha ya Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi. Zippora Pangani kueleza kuwa nishati ya mafuta ya taa itapatikana haraka iwezekanavyo kutokana na bohari ya taifa kupungukiwa na nishati hiyo lakini bado haijajulikana ni lini nishati hiyo itapatikana mjini Bukoba.
Uchunguzi uliofanywa na Blog hii takribani mwezi mmoja sasa, Manispaa ya Bukoba inakabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa nishati hiyo kutokana na vituo vyote vinavyouza mafuta kukosekana kabisa.
Pamoja na baadhi ya wauzaji wa nishati hiyo, hueleza wateja wao kuwa mafuta yako njiani yanakuja ambapo nayatarajiwa kufika muda wowote katika uchunguzi umebaini ni kama danganya toto kwani hata wao hawajui mafuta hayo yatapatikana lini licha ya malori hushusha mashehena ya mafuta ya petroli na dizeli kila kukicha
Katika kuonekana kuwa nishati hiyo imeadimika kabisa katika manispaa ya Bukoba,Juni 17, mwaka huu  usiku baadhi ya wakazi wa mjini hapa walionja joto la jiwe baada ya nishati ya umeme kukatika saa 9 alasiri hadi kesho yake saa 2 uliporudi ambapo baadhi yao walitumia tochi za simu katika nyumba zao baada ya kukosa mafuta ya taa.
Hata hivyo kwa sasa inalezwa kuwa hali ni mbaya sana kwa wananchi waishio vijijini, ambao hutegemea zaidi nishati ya mafuta kwa matumizi ya kapata mwanga ndani ya nyumba zao nyakati za usiku.

No comments:

Post a Comment