Mdau wetu wa gospel kitaa kama tulivyokuhabarisha wiki iliyopita kuhusiana na mchekeshaji maarufu nchini kijana Masanja Mkandamizaji wa kundi la Orijino Comedy kutoa video yake ya kwanza ya gospel inayoitwa ''Hakuna Jipya'', GK imefanikiwa kupata wimbo mmoja uliobeba album hiyo wa Hakuna jipya, basi imeona vyema kuuweka hapa ili wadau wenzetu ambao wapo nje ya nchi au mikoani bado hawajapata video hiyo wanaweza kuangalia angalau wimbo huu mmoja wa utangulizi uliowekwa kwenye mtandao wa YouTube.
Masanja mwenyewe kama ilivyokawaida yake katika mahojiano kupitia kipindi cha gospel celebration kinachorushwa na Wapo Radio Fm kila siku za jumamosi kuanzia saa 5 hadi saa saba mchana kikiongozwa na kijana Silas Mbise, Masanja a.k.a Mchungaji mtarajiwa akizungumzia video hiyo ameruhusu wale wezi wa kazi za wasanii kuiba watakavyoweza hadi Mungu mwenyewe aone kweli injili imefika itakavyo ila katika kuiba kwao amewataka wasiziweke uwani tu, ila wanaweza kukopi watakavyo jambo ambalo aliwaachia vicheko wasikilizaji waliokuwa wakisikiliza kipindi hicho jumamosi iliyopita.
No comments:
Post a Comment