Waombolezaji
wakiwa katika msiba wa marehemu Willy Edward nyumbani kwao Molotonga,
Mugumu Mjini, Serengeti, mkoani Mara, leo
Waombolezaji
wakiwa wamejipanga foleni tayari kwenda ktuo heshima za mwisho kwa
mwili wa marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda (katikati), akiwaongoza
baadhi ya wahariri kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu
Willy Edward wakati wa maziko yaliyofanyika Molotongo,
Mugumu.
Baba wa
marehemu Willy Edward, Edward Ogunde akilia baada ya kutoa heshima za
mwisho kwa nmwili wa mwanawe
Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
marehemu Willy Edward.
Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Jacquiline Liana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
Willy Edward nyumbani kwao marehemu Molotonga, Mugumu Mjini.
Mkuu wa
Wilaya ya Serengeti, Kapteni mstaafu James Yamungu akitoa heshima za mwisho kwa
mwili wa marehemu Willy Edward.
Mjane wa
aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward,
Rehema akimbusu mumewe wakati wa kuuaga muda mfupi kabla ya maziko
nyumbani kwao Molotonga, Mugumu Mjini, Serengeti
jana.
Jeneza lenye
mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward,
likiwekwa kaburini wakati wa maziko yaliyofanyika nyumbani kwao Molotonga,
Mugumu Mjini, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo akiiongoza familia ya
marehemu Willy Edward kuweka udongo kwenye kaburi wakati wa maziko.
Watoto wa
marehemu Willy Edward, Colman na Careb wakiweka shada la maua kwenye kaburi
la baba yao.
Mdogo wa
marehemu Willy Edward, Essey Ogunde (kushoto) na kakao, wakiweka shada la
maua
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda (katikati), akiwaongoza
baadhi ya wahariri kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu
Willy Edward wakati wa maziko yaliyofanyika Molotongo,
Mugumu.
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo (kushoto) na Askofu John Adiema wa Dayosisi ya Rorya
wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Willy
Edward.
No comments:
Post a Comment