Wednesday, April 30, 2014

Ajali ya basi la A.M Tabora

Askari Polisi Kitengo cha usalama barabarani wakiuchukua mwili wa mtoto aliyegongwa na basi la kampuni ya A.M maeneo ya Ipuli Mnadani ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza,katika ajali hiyo watu kadhaa wamejeruhiwa.
Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya
Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.
Wananchi wakishuhudia mwili wa mtoto aliyegongwa na basi hilo ambapo walishauri Serikali iliifungie kampuni hiyo ya A.M kuleta mabasi mkoani Tabora ambayo walidai kuwa ni mabovu na yanausalama mdogo kwa wasafiri.
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika  kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu


 Na Mwandishi wetu Tabora.
Kufuatia kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama kwa wasafiri na wapita njia.

Wananchi hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.

Aidha wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa wa Tabora.

Wameitahadharisha Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima. 

Mambo hayo ya sherehe za Muungano miaka 50

1Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili mwaka 1964 watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo viongozi mbalimbali na marais wa nchi mbalimbali za Afrika na wawakilishi wa nchi mbalimbali pia katika mataifa mbalimbali ya ulaya, Fullshangwe iko kwenye eneo la tukio ikikuletea moja kwa moja matukio  na maelezo zaidi ya picha hizi yatakujia baadae kwa sasa endelea kuangalia picha.(PICHA NA KUKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA UHURU) 234578910111214151617181920

Tuesday, April 22, 2014

Maandalizi ya uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa mkoani Kagera yapamba moto


 Kundi la halaiki ya watoto wapatao 600 wamepikwa wakaiva yote ni hapo Mei 2, Kaitaba Mwaka huu
 Tuko tayari kuupandisha Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro.

















Monday, April 7, 2014

Polisi wa Uganda wazua tafrani mpakani mwa Tanzania na Uganda, waingia nchini kinguvu wananchi wampora mmoja wao silaha ,RPC agoma kuzungumzia

Na Theonestina Juma, Bukoba KATIKA hali isiyo ya kawaida, polisi wanne wenye silaha kutoka nchini Uganda wameingia nchiniTanzania upande wa Mutukula kinguvu na kuanza kurusha risasi ovyo na kuwajeruhi watu wawili. Akizungumza na blog hii njia ya simu, Mkuu wa wilaya ya Missenyi, Kanali Issa Njiku alisema tukio hilo la aina yake lilitokea Aprili 6, mwaka huu saa 11.30 jioni. Alisema wananchi wawili waliojeruhiwa katika tukio hilo la polisi wa nchini Uganda kurusha risasi ovyo mmoja ni raia wa Tanzania ambaye ni mtu mzima na mwingine ni mtoto raia wa nchini Uganda. Kanali Njiku alisema chanzo cha polisi hao kuingia nchini kwa nguvu ni kutokana na kile kinachoelezwa na wao kuwa walikuwa katika msako wa kukamata pikipiki za wizi Mbarambara nchini mwao. Alisema katika harakati hizo, walimkamata mwizi mmoja aliyeiba pikipiki ambapo katika mahojiano yao alikiri kuiba na kwamba pikipiki hiyo ameiuza nchini Tanzania upande wa Mtukula. “Naweza kusema kuwa ni katika hali ya polisi kujitafutia tu riziki, polisi hao wanasema kuwa walikuwa wamemkata mwizi aliyewataka waje Tanzania akawaoneshe mtu aliyemuuzia pikipi alioiba, walifanya hivyo bila kufuata utaratibu wan chi husika”alisema. Alisema polisi hao walipofika katika kuzuizi cha mpaka wa Tanzania na Uganda, walianza kufyatua risasi ovyo, jambo lililowalazimua wananchi upande wa Tanzania kuwavamia kwa lengo la kutaka kuwanyang’anya silaha. “Katika tukio hilo, ilikuwa ni purukushani, wananchi waliwavamia polisi hao waliokuwa wakirusha risasi kwa lengo la kuwanyang’anya silaha ambapo walifanikiwa kumkamata polisi mmoja lengo ilikuwa kuwadhibiti wasiendelee kurusha risasi ndipo risasi ziliwapata watu hao na kuwajeruhi”. Hata hivyo, alisema polisi watatu walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao pamoja na silaha zao na mmoja ndiye walifanikiwa kumkamata ambapo hawakuweza kumdhuru. Alisema Polisi wa Uganda waliohusika katika tukio hilo, si wale wanaoishi maeneo ya mpakani hapo, bali ni kutoka Mbarambara. Alisema Mtanzania alijeruhiwa mkono wake wa kushoto na Mganda ambaye ni mtoto amejeruhiwa mguu wa kushoto ambapo wote wamelazwa katika kituo cha afya cha Bunazi na hali zao zinaendelea vizuri. Alisema kutokana na tukio hilo, taari kamati ya ulinzi na usalama kutoka wilaya jirani zote zinazopakana zilikaa jana usiku kujadili suala hilo ambapo polisi waliohusika wamekamatwa. Aidha kwa sasa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa unaosubiriwa kukaa kujadili suala hilo. Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, George Mayunga alipoulizwa na gazeti hili kuhusu tukio hilo, alikiri kutokea na kusema kuwa hawezi kulizungumzia kwa vile linashughulikiwa na vyombo vya juu. “Suala la Mutukula siwezi kulizunguzia kwa sasa, muda wake muafaka utakapofika nitalizungumzia, lakini kwa leo hapana linashughulikiwa na ngazi za juu’alisema. Kutokana na hali hiyo Kamanda huyo hakuwa tayari kutaja hata majina ya majeruhi wa tukio hilo. Kwa utaratibu, kama nchi jirani inamtafuta mhalifu anapaswa kufuata utaratibu wa kuwasiliana na polisi wa nchi husika kufanya upelelezi wake na kumkata mtuhumiwa huyo na si polisi kutoka nchi nyingine kuingia kinguvu katika nchi husika bila taarifa. Mwisho.