Monday, December 31, 2012

Funga mwaka Kagera, mwalimu ajitia kitanzi kisa msongo wa mawazo



Na Theonestina Juma, kyerwa
MWALIMU wa shule ya msingi Mushisho Wilayani Kyerwa  mkoani  Kagera amejinyonga kwa kujitundika juu ya mti na kuacha ujumbe uliosema kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na msongo wa mawazo yanayomkabili.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa polisi mkoani kagera, Phillip Kalangi tukio hilo limetokea Desemba 30, mwaka huu saa 4 asubuhi wilayani humo.
Mwalimu aliyejinyonga kwa msongo wa mawazo amejulikana kwa jina la Medadi Rwabiga ambapo jana hiyo alionekana akiwa amejitundika kwenye mti uliokuwa karibu na nyumba yake.
habari zinadai kuwa wakati mwalimu huyo alichukua uamuzi wa kujitia kitangazi, mke na watoto wake walikuwa wameenda kanisani. 
Imeelezwa kuwa tukio kama hilo la mwalimu huyo kutaka kujiua kwa kujinyonga si mara ya kwanza, kwani mapema mwezi Desemba mwaka jana alifanya jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa dawa ya kuoshea mifugo.
Hata hivyo katika jaribio hilo mwalimu Rwabiga hakufanikiwa kujiua kwani aliwahishwa hospitalini na kupewa dawa na kuondoa sumu aliokuwa amekunywa kwa muda huo.
Hata hivyo katika kuonesha kuwa bado alikuwa na dhamira hiyo ya kutaka kujiua ilitimia hapo jana alipoamua kuchukua kamba na kutundika juu na mti na kujinyonga.
Habari zaidi zinasema kuwa mwili wa mwalimu huyo ulichelewa kuondolewa katika eneo la tukio, kutokana na  tatizo la daktari kupatikana mara moja.
Hata hivyo  kwa upande wa Kamanda Kalangi alisema hadi sasa hawajajua chanzo kilichomfanya mwalimu huyo kuchukua jukumu hilo nzito la kujinyonga na kwamba bado uchunguzi unaendelea.
“Jana kulikuwa na tatizo la daktari na hivyo leo Desemba 31, mwaka huu ndiyo daktari amepatikana na tayari polisi wako katika eneo la tukio kuufanyia uchunguzi mwili wa daktari”alisem na kwamba mwalimu Rwabiga ameacha watoto wanne na mke mmoja.
mwisho

Sunday, December 30, 2012

Rais Kikwete amtembelea padri Ambrose hospitalini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
PICHA NA IKULU

Saturday, December 29, 2012

Mwanafunzi Daktari aliyebakwa na wanaume sita nchini India afariki dunia Singapore

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Madaktari katika hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore wametangaza kuwa mwanamke aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia kubakwa na kundi la wanaume sita mjini New Delhi nchini India amefariki dunia.
  

Hospitali ya Mount Elizabeth ya nchini Singapore alikokuwa akitibiwa mwanamke aliyebakwa nchini India
Hospitali ya Mount Elizabeth ya nchini Singapore alikokuwa akitibiwa mwanamke aliyebakwa nchini India
haveeru.com.mv
Taarifa hizo za simanzi zinaeleza kuwa mwanamke huyo daktari mwanafunzi,ambaye tukio la kubakwa kwake lilizusha maandamano makubwa nchini mwake, amefariki kwa amani mapema asubuhi leo Jumamosi.

Akielezea kwa masikitiko taarifa hizo mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Kelvin Loh amesema kuwa pamoja na jitihada zote zilizofanywa na timu ya wataalamu sita kuhakikisha kuwa hali yake inaimarika, juhudi hizo zimegonga mwamba na hatimaye majira ya saa 10 na dadika 45 alfajiri hii leo amefariki dunia.
Kufuatia taarifa za kifo hicho waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa hizo na kuahidi kuchukua hatua madhubuti dhidi ya waliotekeleza unyama huo.

Friday, December 28, 2012

Disko toto ruksa Kagera nyakati za sikukuu



Na Theonestina Juma, Kagera
WAKATI baadhi ya Makamanda wa Jeshi la polisi wakipiga marufu ya disko toto, kwa mkoa wa Kagera hali iko tofauti kutokana na kuruhusiwa kuwepo nyakati za sikukuu
Kamanda wa polisi Mkoa Kagera, Phillip Kalangi akizungumza na waandishi wa habari alisema disko toto linaruhusiwa nyakati za sikukuu mkoani Kagera ambapo waandaji wanatakiwa kufuata utaratibu na maagizo yaliotolewa na Jeshi hilo.
Alisema wandaaji wa disko toto wanatakiwa kuaandaa sehemu ambayo iko wazi, ambayo haiwezi kuhatarisha maisha ya watoto.
Alisema watu hao wanatakiwa kuwa na kibali maalum kwa wale wanaoaandaa disko toto.
Alisema sababu ya kuhjitaji swehemu ambapo pako wazi ni kutokana na baadhi ya maeneo kutokuwa na miundo mbinu.
“Maeneo ya kufanyia disko toto lazima pawe pawazi ili likitoea tatizo lolote linakuwa rahisi kutoa msaada na watoto wasijazwe kupita kiasi, lazima muandaaji awe na kipimo, idadi ya watoto aliowalenga’alisema.
Hata hivyo katika uchunguzi wa gazeti hili katika kata ya Katoma kuliezewa kumbi kwa kutumia makuti kwa ajili ya kuendeshea disko toto.
Mwisho.

Umoja wa makanisa ya Kikristo yandaa mkesha wa mwaka mpya kuiombea taifa Amani , uwanja wa Kaitaba



Na Theonestina Juma, Kagera
UMOJA wa makanisa ya kikristo mkoani Kagera umesema hawafurahishwi na hali halisi inayoendelea hapa nchini na kwamba, jibu pekee ni wananchi kumrudia Mungu na kutoruhusu kugombanishwa na ukoloni mamboleo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mratibu wa siku ya maombi ya kuiombea taifa usiku wa  mkesha wa mwaka mpya unaotarajiwa kufanyika Desemba 31,mwa huu katika uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku, Mchungaji wa kanisa la Tanzania Fellowship of churches Jijini Dar Es Salaam,  Paulo Kashaga  wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa juu ya maandalizi ya siku hiyo.
 Alisema “kamwe sisi viongozi wa dini hatufurahishwi na mambo yanayoendelea hapa nchini, ya kuchomewa makanisa, viongozi wa dini kupigwa risasi, kumwagiwa tindikali,haya mambo hayakwepo hapo awali hapa nchini mwetu, …. Kwa sasa yanatengezwa (artificial),  yanachochewa na ukoloni mambo leo, viongozi wa dini nao wasilikubali hili”.
Kutokana na kutofurahishwa na vitendo hivyo, tayari baadhi ya viongozi wa dini katika nafasi zao wameshaandika barua nyingi na kuziwasilisha serikali kwa kutoa mapendekezo yao nini kifanyike na hii ni kutokana na mambo mengine yanayohitaji marejeo.
Mchungaji Paulo ambaye kitaalum ni mhandishi na  ni mwanajeshi Mstaafu (JWTZ), alisema waumini wa kikristo na wananchi kwa ujumla kamwe wasikubali kuyumbishwa na ukoloni mambo leo, ambayo yanaingilia kupitia kuwagombanisha watanzania kidini ili waweze kupata nafasi ya kuchuma maliasili ya nchi.

Pichani ni viongozi wa dini wanaoratibu mkesha wa mwaka mpya wa maombi ya kuiombea taifa amani, kutoka kulia ni Mwalimu Ruben, kati kati ni mchungaji Paulo Kashaga na kushoto ni mchungaji Peter Benjamin.

"Malumbano yanayoibuka kwa sasa hapa nchini ni kutokana na kugombanishwa, na kama watalitambua hilo na kukataa kugombanishwa wagombanishaji hao hawawezi kufanikiwa na pia yanatokana na watu kuacha maadili ya  ki-Mungu na kutawaliwa na utandawazi ambayo nchi haiwezi kukwepa”alisema mchungaji huyo.
Mchungaji Paulo alisema maombi pekee kwa wakristo ndiyo silaha kubwa ya kutunza amani  na utulivu wa nchi yetu.
Alisema lengo la kuendesha maombi hayo mkesha wa mwaka mpya ni kwa ajili ya kuiombea  nchi amani na utulivu, watawala na vyama vya siasa pamoja na bunge letu, kwa sababu hawataki  masuala ya malumbano yakitokea bungeni ambako ndiko tegemeo la nchi katika kutunga sheria, na kwamba maombi hao yatafanyika katika mikoa 17 ikiwemo na Zanzibar
Akizungumzia juu ya maandalizi hayo, alisema yamekamilika kwa asilimia 100 kutokana na watu wengi pamoja na wafanyabiashara wa mjini hapa wamehamasika kutoa sadaka zao kwa kuchangia uendeshaji wa mkesha huo na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa uwingi kushiriki katika maombi hayo
Alisema siku ya mkesha wa mwaka mpya, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe na kwamba yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kuhusu malalamiko yanayotolewa baadhi ya viongozi kwa kuwa inapendelea dini fulani, mchungaji huyo aliwataka kuachwa kabisa kwa sababu hayana busara kwani serikali inayokuwa madarakani  Mungu anaitambua halijaishi kama kiongozi ni Muislamu ama mkristo .
“Mimi nawaomba viongozi wa dini ,Maaskofu, mashekhe waachane kusema  maneno ya upendeleo kwani hayana busara kabisa , hayampendezi Mungu, tunawaomba Watanzania wananchi kama nchi moja , dunia inatuangalia sisi kama  tuna ukombozi, kwani tunayo madini na rasilimali zetu, mfano kama Geita hawajui zile dhahabu zimetoka wapi”alisema
Mwisho.

Sifa za mwanamke wa kweli mwenye 'moyo wa umama'Lakini zingine ni kandamizi kwa mwanamke

Mwanamke wa kweli mwenye moyo wa umama ametofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamke mwingine yeyote. Mwanamke huyu awe amebarikiwa kupata watoto ama la lakini atakuwa na sifa zifuatazo.
1) Ana upendo wa kweli kwa watu wa nyumbani mwake. Yaani si mbaguzi hata kidogo.Na daima huifanya familia yake kuwa priority. Na kwamwe hutumika kama daraja la kuunganisha familia zote mbili alikotoka yeye na alikotoka mumewe.
2) Ana hekima katika kuyakabili mambo ya nyumbani mwake. Hata siku moja haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake.
3) Ana uvumilivu sana katika jambo lolote lile gumu na daima huona gumu lolote limpatia kama changa moto tu na si kama kosa.
4) Ana siri sana juu ya maisha ya nyumbani kwake daima hukuti mambo ya nyumbani nje watu wakiyajadili.
5) Ni mchapa kazi hodari, tena ambaye hawezi kuruhusu familia yake ikalala njaa kisa baba hajaleta chakula. Ama watoto wasisome shule kisa baba hajalipa ada.
6) Daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake.
7) Siku zote huamka wa kwanza nyumbani, na hulala wa mwisho. huakikisha mambo yote ya ndani yako sawa kabla ya yote.
8) Huwa hadekezi watoto wala haengi watoto katika kazi,huakikisha nyumbani kwake kila mtoto ni mchapa kazi na nidham ya ndani ya nyumba ipo.
9) Si mbishi wala hawezi kubishana na mumewe mbele za watu, kwani ni msikivu sana kwa mumewe na daima humfanya mume kuwa kiongozi na kamwe huwa habadili cheo cha baba.
10) Ni mwepesi wa kukiri makosa yake kwa mumewe na kuomba samahani lakini pia ni mzuri sana kwenye kuremedy makosa yake.
13) Siku zote ni msafi wa mazingira na mwili daima nyumba yake husifika kwa usafi.
14) Mume na watoto wake hujulikana hata wanapoonekana njiani maana yake huakikisha amewavesha vizuri, kinadhifu na watoto wanaheshima sana.
15) Ni mcha Mungu, kwa imani yake. hata kama baba si mtu wa sala lakini yeye huongoza watoto katika ibada kila iitwapo leo.
16) Hupendelea zaidi maendeleo hasa ya kiuchumi na daima hupenda vitu vizuri na hujitahidi sana vipatikane.
17) Si mpayukaji wala mtu wa kisirani nyumbani mwake. Maneno yake huwa yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole.
18) Hupendelea kupika na hujisikia furaha sana akipika kwa ajili ya familia yake. Na siku akipika basi hata watoto husema leo tunakula chakula kitamu manake ni desturi yake kupika chakula kitamu.
19) Humuheshimu sana mumewe, na daima hupenda kuisikia kauli ya mumewe katika maamuzi. siku zote humfanya baba kuwa msemaji wa familia yake na huakikisha kauli ya baba inatekelezwa.
20) Kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule.
Chanzo jamiiforums

Wednesday, December 26, 2012

Mbwa mwitu kulindwa kwa milioni 30 katika hifadhi ya Serengeti

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 
Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Polisi Kagera yafanya kweli yanasa noti bandia zipatazo milioni 10 na nyara za serikali

 Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kufuatia operation mbalimbali lililoziendesha kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani humo, vitu hivyo ni pamoja na viungo vya wanyama mbalimbali vikiwemo meno, pembe na ngozi, bunduki aina ya SMG na risasi zake, pesa bandia na kamba zinazotumiwa na waharifu kutekeleza uharifu, pia kufuatia msako huo zaidi ya bunduki 15 zilizokuwa zinamilikiwa kinyume na sheria zilisalimishwa.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi, akionyesha bunduki aina ya SMG iliyokamatwa kufuatia operation iliyoendeshwa na jeshi la polisi mkoani Kagera iliyopendeshwa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Kagera (kukia) Mwaibambe.


 Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mwaibambe akionyesha pembe za wanyama mbalimbali zilikamatwa na jeshi la polisi kufuatia msako lililouendesha.
Noti bandia zipatazo sh. milioni 10 zilizkamatwa wilayani Karagwe
Silaha mbalimbali zilizosalimishwa kwa hiari kufuatia operation ya jeshi la polisi.

Lulu:-Kanumba alijitabiria kifo chake

MSANII maarufu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), anayekabiliwa na mashitaka ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba, amedai mahakamani kwamba walikuwa wapenzi, walipendana sana lakini hawakuaminiana.
“Siku mbili kabla ya kifo chake alitabiri kifo hicho kwani alinitumia ujumbe unaosema, nitakufa kwa ajili yako, nakupenda sana,” hayo yalikuwa maneno ya Lulu aliyoyatoa Polisi wakati akihojiwa.
Muhtasari huo wa ushahidi ulisomwa jana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi Augustino Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kweka alidai, Sajenti Revonatus aliyechukua maelezo ya Lulu baada ya tukio, alidai lulu alianza uhusiano wa mapenzi na Kanumba Junuari mwaka huu, katika uhusiano wao walikuwa wanagombana kama mtu atapokea simu ya mwenzake.
Alidai Lulu wakati akiwa Mikocheni kwa rafiki yake Ritha, kabla ya kutoka akampigia simu mpenzi wake Kanumba na kumwambia kuwa anataka kutoka, alipofika nyumbani kwa Kanumba alimkuta anazungumza na simu.
Lulu alidai na yeye alipigiwa simu na rafiki yake wa kike, alipotaka kwenda kupokea simu nje Kanumba alimzuia asitoke nje na yeye alitoka nje na ndipo Kanumba alipomkimbiza mpaka barabarani.
Alipomshika akaanza kumpiga makofi na mateke, walipoingia ndani, Kanumba alimtupa kitandani na kuchukua panga chini ya kitanda kisha kuanza kumpiga na ubapa wa panga katika mapaja yake.
“Lulu alikubali kutoa maelezo hayo akiwa peke yake na kwamba alikuwa huru katika uhusiano wake na Kanumba, kwani alikuwa anaenda kulala kwake kila alipokuwa akijisikia kufanya hivyo, lakini hawakuwahi kuishi pamoja.
“Aprili 5 mwaka huu usiku, Kanumba alimtumia ujumbe kuwa ‘you will kill me soo, I love you so much, akamfariji kwa kumwambia kuwa achana na mambo hayo na akawa sawa.
“Tarehe 6, Kanumba alimpigia simu na kumwambia anatarajia kusafiri kwenda Marekani April 14, mwaka huu amletee zawadi gani naye akamjibu zawadi yoyote,” alidai Kweka wakati akisoma muhtasari wa ushahidi.
Alidai walikuwa wanapendana lakini hawaaminiani wakiwa mbali, kwani Kanumba alikuwa na wivu wa kimapenzi na alikuwa anasema anamdharau.
Mshitakiwa alidai hakumsukuma Kanumba, Kanumba alivyompiga na ubapa wa panga alilitupa chini na kuanza kuhema kwa hasira ambazo hakuwahi kuona tangu wawe wapenzi.
Alidai mshitakiwa alijigonga kisogoni katika ukuta na kuanguka chini, lakini alipomuona kama anataka kunyanyuka, alikimbilia chooni na kujifungia ndani, baada ya muda aliona Kanumba anatokwa na povu ndipo alimwagia maji na kutoka nje kwenda kumwita mdogo wake Seth.
Lulu alipopewa nafasi ya kusema chochote katika Mahakama ya Kisutu, alisema hana chochote cha kusema.
“Nawatakia mafanikio mema huko Mahakama Kuu katika kesi hii, nawashukuru mawakili wote, waandishi wa habari na wananchi wote ambao tumeshirikiana pamoja, Lulu utarudi gerezani mpaka utakapoitwa Mahakama Kuu,” alisema Hakimu Mmbando.
Upande wa Jamuhuri utawasilisha mashahidi tisa na vielelezo vya ushahidi wa ramani ya eneo la sehemu alipofia Kanumba, ripoti ya ukaguzi wa daktari na maelezo ya onyo ya Lulu aliyopewa.
Mawakili wa utetezi ni Fuljensi Masawe, Kenedy Fungamtama na Peter Kibatala.
VN:F [1.9.22_1171]

Afisa wa Takukuru aliyeuawa juzi Bhoke Ryoba azikwa leo Rorya

MAMIA ya wakazi wa Wilaya ya Rorya, Tarime na Mkoa wa Mara kiujumla wamejitokeza kwa uwingi kumzika aliyekuwa Afisa wa TAKUKURU Bhoke Ryoba (34) aliyeuawa na mtumishi mwenzake kwa kumfyatulia risasi kisogoni.
Maziko hayo yametawaliwa na simanzi kubwa katika kijiji cha Kiterere kata ya Bukwe wilayani Rorya, ambapo aliendesha misa ya maziko hayo ni Padri kutoka katika Kanisa Katoliki parokia ya Kowak.
Mumewe Bi. RYOBA , BW.Charles Gibore,amesema kifo cha mkewe kimegubikwa na utata mwingi ,  pamoja na mambo mengine alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt Edward Hoseah(pichani) na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kubaini ukweli.
“Mke wangu aliuawa na mfanyakazi mwenzake na tukio hilo limegubikwa na utata ambao Takukuru na Polisi ndiyo pekee wanaoweza kutupa ukweli,” alisema Gibore nje ya chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.
Gibore alieleza kuwa mkewe huyo aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili katika tafrija ya kuagana na kupongezana na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Takukuru waliokuwa wamepandishwa vyeo, tafrija ambayo Bhoke alipewa zabuni ya kupika chakula.
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dr. Edward HoseaAlisema pia mkewe aliombwa pia awapatie wenye sherehe hiyo, vijana wawili wa kuwachomea nyama… “Vijana hao walikwenda asubuhi ukumbini ili kuandaa eneo la kuchomea nyama, huku Bhoke akiwa bado nyumbani akiandaa chakula,” alisema Gibore na kuongeza:
“Wale vijana walinieleza kwamba baadaye saa 8:30 mchana, Bhoke na wenzake walifika ukumbini na kuwakuta vijana wawili wanaofanya nao kazi wakinywa pombe, huku wakichezea silaha aina ya bastola kujaribu shabaha.”
“Vijana hao walifyatua risasi juu na ndipo muuaji alipompiga kichwani marehemu katika jicho na mauti yalimfika muda mfupi,” alisema.
Alisema baada ya hapo muuaji huyo alitoweka kisha kujisalimisha mwenyewe katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Temeke, Chang’ombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha mtuhumiwa huyo kujisalimisha na kisha kushikiliwa kituoni hapo na kueleza kuwa amekuwapo hapo Jumamosi iliyopita.
Kamanda Kiondo alisema pamoja na mtuhumiwa huyo kujitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Takukuru, polisi wanaendelea kuchunguza ili kubaini ukweli wa taarifa hizo.
“Tunaendelea kumshikilia hapa na uchunguzi utakapokamilika tutamfikisha mahakamani kwa taratibu nyingine za kisheria,” alisema Kiondo.
Marehemu Bhoke Ryoba alizaliwa Juni 18, 1978 katika Kijiji cha Kiterere, Wilaya ya Tarime mkoani Mara na anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao. Ameacha watoto watatu; Doloresy (10), Dolrisy (4) na Dolrick Gibore ambaye ana mwaka mmoja.
VN:F [1.9.22_1171]
Bi. RYOBA alipata elimu yake ya sekondari Mwanza sekondari na kidato cha tano na sita shule ya sekondari ya Mkwawa Iringa.
Bwana Ametoa Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe, AMENI

Tuesday, December 25, 2012

Mbunge wa Viti Maalum, Bernedetha Mushashu asherekea X-Mas na watoto yatima Bukoba

Mbunge Viti Maalum CCM,Bernedetha Mshashu akiwapatia zawadi ya vifaa vya kwa watoto yatima wanaotoka katika kata ya Katoma 
 Watoto wakipewa zadi ya X-Mas

 Hawa watoto wanaangalia vifaa vya shule walivyopewa na Mbunge wao 

 Mlemavu wa kutambaa akifurahia kitenge alichpewa zawadi na Mbunge Mshashu
 Hapa Bi. Mshashu akimfunika  kwa kitenge mlemavu wa viungo Bi.Rahima Rarmu


 mtoto Diana Festo (13) aliyefaulu kwenda sekondari ya Katoma akifurahia zawadi alipewa na Mbunge.Mtoto Diana alipata ajali ya kugongwa na gari mwaka 2006 akiwa darasa la kwanza na kupata ulemavu wa maisha.


 Bi Mshashu akisalimia na Mwenyeiti wa chama cha walemavu viziwi Bi. Judidh Kashulija, chama hicho kilialikwa na Mbunge katika kusherekea siku ya X-mas iliofanyika nyumbani kwake.


 Baadhi ya watoto waliohudhuria katika sherehe hizo.
 Sehemu ya walemavu  Viziwi waliohudhuria kwenye sherehe hizo huyo  aliyebeba mtoto ni Bi. Delphina Juston akiwa amebeba mwanae Alistidia   Ajuna Jovinus aliyevaa  baluzi nyeupe ni Jovitha Jonathan katibu wa chama cha wanawake Viziwi Kagera

 Watoto wakiserebuka
Walemavu Viziwi nao hawakuwa nyuma kuburudisha na nyimbo za ngoma za kienyeji

 Hapa wanawake viziwi wakijitambulisha
 Kati kati ni Mbunge Viti maalum, Bi. Mshashu na upande wake wa kushoto ni mumewe, Bw. Mshashu
 Ilifika muda wa shanpein, aliyeoongoza zoezi hilo ni Bi. Anna
 Kikundi cha Ubunifu cha Katoma kinachofadhiliwa na Mbunge huyo kikitoa burudani



Hawa ni watoto ndugu walipewa vifaa vya shule.watoto hawa ni yatima , kutoka  kulia ni kaka yao mkubwa mabinti hawa, Muctary Amari (12), anayemfuatia ni Nairath Amari (10), wapili kutoka kushoto ni Isha Amari (9) na wa kushoto ni Sawia Amari (8)
 Mwenyekiti wa Chama cha wanawake Viziwi, Bi. Kashuliza akipewa zawadi ya kitenge na Mbunge wa Viti Maalum Bi. Mshashu.