Kapumzike kwa amani Wille wa Ogunde
Salaamu wasomaji, Moyo naupiga konde,
Sihitaji hata maji, kama viazi
mviponde,
Nimejawa na simanzi, Kifo cha kaka Ogunde,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa
Ogunde.
Tusimlaumu Mungu, sote tulio waungwana,
Najua tuna uchungu, yowe ni kwamaulana,
Mola angetupa fungu, kifo siwe cha kijana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa
Ogunde.
Twasema kasitukizwa, Wille kaenda kijana,
Alipo kuja hatukuulizwa, tulimwona tu
mvulana,
Mungu we ndo muweza, kifo leo
twakimbizana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa
Ogunde.
Mwaka ule 74 machi saba, Wille ukaiona
dunia,
Leo amegonga siku ya saba, ukamtwaa hii
dunia,
Tena tarehe kumi na saba, Wille kaiga
dunia,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa
Ogunde.
Wille ulilia kaka, siku uliyo iona dunia,
Pinto, Mroki na Kisaka, sasa zamuyetu
kulia,
Wengi wanatafuta kichaka, lini nao
watatwaliwa,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa
Ogunde.
Pigo la wana habari, Tanzania na Afrika pia
Hakika kifo ni bahari, hakuna ajuae
ilikoanzia,
Kifo ni jemedari, Wille amesha twalia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Salamu kawape jalia, wote walo kutangulia,
Mwakiteleko alotulia, na wote wana
familia,
Wanahabari tunalia, Wille Ogunde
kutangulia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Father Kidevu tamatia, nangoja nami kufuatia,
Father Kidevu tamatia, nangoja nami kufuatia,
Siku itapo fikia, hakuna atakae bakia,
Kifo kitendawili, Mola ndie atakae
kitegua,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Mroki Mroki a.k.a Father Kidevu
0717002303/0755 373999
No comments:
Post a Comment