Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akifanyiwa vipimo vya awali
kabla ya kuchangia damu. Kulia Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama
Bi. Edith Senga.
Na.Mwandishi
wetu
Umoja
wa Mataifa umetoa wito kwa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi
kujitolea damu ili kufanikisha azma ya serikali ya kuwa na damu ya kutosha
katika benki ya akiba ya damu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika kituo cha kijitolea damu kilichopo katika
zahanati ya UN iliyopo Kinondoni, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic
Kacou amesema Umoja huo unashirikiana bega kwa bega na serikali katika
kuhamasisha kampeni ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Katika
kufanikisha kampeni ya kitaifa ya Kujitolea Damu, Umoja wa Mataifa umeweka
utaratibu wa kuwa na vituo katika sehemu mbali mbali ambapo wananchi watakuwa
wakijitolea damu, ambapo kwa kuanzia leo kituo kipo katika klinik ya UN ambako
kwa kuonyesha mfano Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou
amejitolea damu.
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu akizungumza leo amesema kesho tarehe 14 June 2012 ambayo ndio kilele cha Siku ya Kujitolea Damu Duniani,
shughuli hiyo itafanyika katika Ofisi za Shirika la Afya Duniani – WHO zilizopo
mkabala na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
Aidha
amewataka wananchi jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha
lengo la Siku ya Kujitolea Damu Duniani, na kuwatoa hofu kuwa sio kweli kwamba
ukijitolea damu unapimwa virusi vya ukimwi au damu yako
itapungua.
Viongozi
katika ngazi mbalimbali na watu wote mashuhuri wanatakiwa kutumia nafasi
walizonazo kuhamasisha watu kuchangia damu.
|
No comments:
Post a Comment