Wednesday, June 6, 2012

RC : Massawe day " Nafasi ya tatu haijaniridhisha, 2013 tutakuwa wa kwanza

NI jambo la kujivunia, ni kama ndoto, lakini yote ni sifa kwa Kanali Fabian Massawe kuwezesha Manispaa ya Bukoba kuona mwezi kwa kushika nafasi ya tatu kwa usafi kitaifa.
Alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera  na Rais Jakaya Kiwete na kuhamishia makao yake makuu katika Manispaa ya Bukoba, kila mkazi wa Bukoba alikuwa tumbo moto kutokana na mazoea yao walikokuwa nayo ya kuwa na desturi ya kutofanya usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Lakini ikumbukwe kuwa tangu kuanzishwa kwa wilaya ya Bukoba, ikaja  halmahsauri ya mji wa Bukoba hatimaye Manispaa ya Bukoba, haijawahi tokea hata siku moja kushika nafasi za juu katika suala la kulinda mazingira, mwaka huu ni bahati yetu'Massawe Day".
Wakati Kanali Massawe akianza kuunda kamati ya kufuatilia suala ya usafi, kila mkazi wa Bukoba alianza kumchukia hadi kufikia hatua ya baadhi ya wanasiasa kuanza kumshutumu hadhari kwa madi kuwa nawaingilia hasa ile 'kambi ya seneta soko kuu'.
Lakini Massawe alijua anafanya nini na alitaka kuwaonesha wanabukoba kuwa kilio cha chura hakimzuii ng'ombe kunywa maji, aliendelea na jitihada zake pamoja na kundi lake.
Kila alhamisi Kanali Massawe na timu yake huonekana mitaa ya Bukoba wakiwa na kipaza sauti,wameingia katika mavazi yamatrack suti, mikono wakibeba mifekeo, mifagio wakizunguka huku na kule huku baadhi ya watu mashuhuri kwa uchafuzi wa mazingira wakikwepeshana nao katika maeneo ya vichochoni wakionesha dhahidhiri kutotaka kuinama kufanya usafi.
Shuguli nyingi husimama kwa saa kadhaa kwa lengo la kuenzi siku hiyo tukufu la Alhamisi kwa kufanya usafi.
Matokeo yake kwa mwaka huu umepatikana.Sijasikia hata mwana Bukoba anayezungumzia nafasi walioipata kitaifa ya kudumisha usafi, licha ya kuwa wanajulikana kwa watu wengine kuwa ni wadumisha usafi... lakini kumbe....
Kwa sasa kila sehemu ukipita utasikia baadhi ya watu wakisema Massawe day kaibuka mshindi wa tatu... wala hawasemi tumekuwa wa tatu kwa usafi kwa upande wa manispaa hapa nchini. Nashindwa kwa waelewa watu hawa ina maana leo hii Kanali Massawe akiondoka  Bukoba na usafi wa mazingira nao utaondoka?
Kwa taarifa yenu, nadhani mwakani sasa ndiyo kuna kazi, kwani Massawe Day anasema hajui ni kwa nini Manispaa ya Bukoba isiwe ya kwanza kwa usafi, kwani namba tatu bado haijamfurahisha licha ya mtu wa kwanza kwa utunzaji wa mangira kwa mwaka 2012 ametoka wilaya ya Karagwe alikoanzishia usafi wa mazingira.
Haya jamani leo ni Alhamisi siku ya Massawe Day kwa upande wa Manispaa ya Bukoba, kila mmoja achacharike kwa nafasi yake katikakusafisha mazingira yake, tunza mazingira yakutunze, mazingira ndiyo uhai wa mwanadamu.

No comments:

Post a Comment