Friday, June 8, 2012

kutowashirikisha wananchi usimamizi wa rasilimali chanzo cha umasikini Nchini-Masinde

Bukoba
MWENYEKITI wa bodi ya wadhamini Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ), Bw. Sylvester Masinde amesema chanzo  cha umasikini nchini ni kutokana na mfumo wa utawala usioshirikisha wananchi  ambao hausimamii kikamilifu rasilimali za nchi.
Bw.Masinde alitoa kauli hiyo  jana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika uwanja wa  Mayunga mjini hapa uliohudhuriwa na mamia wa wakazi wa Manispaa ya Bukoba
Alisema mfumo wa utawala usioshirikisha wananchi wa kusimamia rasilimali za nchi umejengeka na usimimizi mbovu wa utendaji na kufanya mfumo ulipo wa mamalaka zote kuwa jijini Dar-es- Salaam.
Alisema  msingi wa ufisadi ni utawala mbovu na wanachi wenyewe na kwamba serikali ilianza kuwakumbatia mafisadi kwa kuwastaafisha wakidai ni kwa maslahi ya umma na wakati huo wakilipwa kinuua migongo bila kujua kuwa wanafilisi nchi.
Hivi  mtumishi amewaibia wananchi bado una mstaafisha kwa madai ya maslahi ya umma na kumpa pesheni kama sio kuwaibia wananchi ni nini?alihoji Masinde huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliofurika katika uwanja huo.
Katika hatua nyingine, Bw.Masinde alionesha kusikitishwa  na hali ya mkoa wa Kagera kuzidi kurudi nyuma katika sekta ya mendeleo badala ya kupiga hatua kama ilivyo kwa mikoa mingine hapa nchini..
Alisema dhana ya maendeleo ni kuongeza vitu vipya lakini katika mkoa wa Kagera vitu vya zamani vilivyokuwepo ndivyo bado vinapatikana hadi hivi sasa jambo linaloonesha wazi kuwa  mkoa huo badala ya kwenda mbele unarudi nyuma tu kimaendfeleo.
Bw. Masinde ambaye aliwahi kuishi mkoani hapa akiwa Mkurugenzi wa maendeleo  katika miaka ya 1980 alisema wananchi wanatakiwa kujizatiti katika harakati za kujiletea maendeleo ili mkoa uweze kusonga mbele.

 Alisema  mwaka 1983 serikali ya Tanzania na Italia ulileta umeme katika mkoa wa Kagera kutoka Uganda wakati  huo Profesa Mark  Mwandyosa akiwa kamishana wa umeme lakini uongozi wa wakati huo akiwemo Meya Mstaafu wa Manispaa ya BUkoba Bw. Samwel Luangisa waliweka vikwazo lakini uliwalazimu kupambana mpaka umeme ukafika Kagera.

Alisema sababu mojawapo uliwafanya kufanikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi  na kuwajibika kwa juhudi na maarifa kwa maslahi ya wananchi waliokuwa wakiwatumika ambapo kwa sasa hali ni tofauti.

Alisema serikali iliyoko madarakani kuwaweka wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya ni njia ya kuwalaghai wananchi kwa kuwadanag’anya kuwa ni Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za Wilaya na Mikoa.
Hivi  majeshi yote yanawajibika katika idara zao nani aliwaambia kuwa kamanda wa polisi mkoa anawajibika kwa mkuu wa mkoa kiutendaji?alihoji mwenyekiti huo.

No comments:

Post a Comment